Sh bilioni 19.7 kutumika katika ukarabati wa Uwanja wa Uhuru nchini Tanzania

(CRI Online) April 28, 2024

Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo nchini Tanzania, Gerson Msigwa, amesema jumla ya Sh bilioni 19.7 zitatumika kukarabati Uwanja wa Uhuru ulioko jijini Dar es salaam.

Bw. Msigwa amesema hayo katika hafla ya kusaini mkataba wa kuanza kwa ukarabati wa uwanja huo iliyofanyika Ijumaa jijini Dar es Salaam, ambao utatekelezwa na Kampuni ya Uhandisi na Ujenzi wa Reli ya China (CRCEG) na utakamilika baada ya mwaka mmoja.

Uwanja wa Uhuru ni moja ya viwanja vilivyo katika mpango wa viwanja vitakavyotumika katika Michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika mwaka 2027 (AFCON 2027), ambapo Tanzania itakuwa moja ya nchi wenyeji wa michuano hiyo mikubwa zaidi barani Afrika.

Kwa mujibu wa Msigwa, uwanja huo utatumika katika mazoezi ya timu shiriki katika michuano hiyo.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha