Kuupa lebo kwa kuupaka matope uwezo wa uzalishaji wa kijani wa China ni kujifelisha mwenyewe kwa kutazama uhalisia uliopo

(Tovuti ya Gazeti la Umma) April 28, 2024

Kwa miaka tisa mfululizo, China imeshika nafasi ya kwanza duniani katika uundaji na uuzaji wa magari yanayotumia nishati mpya (NEVs).

China imeendelea kushikilia nafasi ya juu katika ukubwa wa soko la betri za nishati kwa miaka minane na kudumisha kwa miaka kumi mfululizo uwezo wa juu zaidi wa kuzalisha umeme kwa nishati ya jua kupitia vifaa vilivyofungwa. Mafanikio haya yanaangazia mchango mkubwa wa viwanda vya uzalishaji bila uchafuzi vya China vinavyostawi katika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi, kuhimiza viwanda kubadilisha muundo wa uzalishaji kuwa wa kijani na wa kutoa kaboni chache, na kutoa mchango mkubwa kwa ajili ya kuleta msukumo mpya wa ukuaji wa uchumi wa dunia nzima. 

Wafanyakazi wakifanya kazi kwenye mstari wa kuunda magari wa kampuni ya magari ya Seres ya China katika Eneo Jipya la Liangjiang, Mji wa Chongqing, Kusini Magharibi mwa China, Aprili 25, 2024. (Picha: Xinhua)

Wafanyakazi wakifanya kazi kwenye mstari wa kuunda magari wa kampuni ya magari ya Seres ya China katika Eneo Jipya la Liangjiang, Mji wa Chongqing, Kusini Magharibi mwa China, Aprili 25, 2024. (Picha: Xinhua)

Licha ya mafanikio haya, watu binafsi nchini Marekani wameupa lebo kimakosa uwezo wa uzalishaji wa kijani wa China kutokana na sera ya ruzuku na nguvu bora iliyotokana na ushindani usio wa haki.

Maoni haya yalipuuza hali halisi ya mambo. Mtu yeyote ambaye ametembelea kampuni za sekta ya nishati mpya ya China mwenyewe na kufahamu historia ya maendeleo ya sekta ya viwanda nchini China atajua kwamba nguvu bora za ushindani za viwanda vya uzalishaji wa kijani vya China katika jukwaa la kimataifa zinatokana na fikra za dhati na juhudi thabiti.

Nguvu bora za ushindani zinatokana na uvumbuzi wa kampuni na taasisi za utafiti na maendeleo ya bidhaa (R&D), na kupata uwezo wa kushindana katika soko kunahitaji miaka mingi.

Kupitia kazi ngumu endelevu, kampuni za magari za China zimepata mafanikio makubwa katika teknolojia za akili mnemba (AI) na za umeme kwa ajili ya NEVs. Kwa mfano, zimetengeneza betri zenye kiwango cha nusu-yabisi zenye kuweza kutumika kwa umbali wa kilomita 1,000 zikiwa zimechajiwa mara moja na majukwaa ya silicon ya voti 800 za juu yenye kuweza kuhakikisha matumizi ya umbali wa kilomita 400 kwa kuchajiwa kwa dakika tano. Zaidi ya hayo, zimeunda sehemu za madereva kwenye magari zenye teknolojia za kisasa zinazojumuisha miundo ya kiwango kikubwa ya AI na NOA ya mjini (Navigate on Autopilot) mifumo ya usaidizi ya kuendesha gari isiyotegemea ramani za usahihi wa juu.

Kwa mujibu wa uchunguzi wake, Tawit Thanachanan, naibu meneja mkuu mwandamizi wa kwanza wa Kampuni ya Kasikornbank ya Thailand, amesema kuwa viwanda vinavyoibukia vya China vimepata nguvu ya ushindani kwenye soko la kimataifa katika miaka ya hivi karibuni kwa sababu kampuni za China zinakumbatia kikamilifu uvumbuzi, utafiti na uundaji wa bidhaa, na kupunguza gharama za uzalishaji. 

Nguvu bora ya ushindani inatokana na China kukamilisha siku hadi siku mfumo wa viwanda na mnyororo wa utoaji bidhaa.

Kwa nini kiwanda kikubwa huko Shanghai kinaweza kuchukua zaidi ya nusu ya uwezo wa kimataifa wa kampuni ya magari ya Tesla? Jibu liko katika ukamilifu na ufanisi wa mnyororo wa viwanda vya uundaji wa magari ya kutumia nishati mpya vya China. Shanghai inatoa chipu na program za mifumo; Mji wa Changzhou wa mkoa wa Jiangsu unatoa betri za nishati; Mji wa Ningbo wa mkoa wa Zhejiang unatoa mashine fungamani za kutengenezea bodi za magari; na katika eneo la Delta ya Mto Changjiang (Yangtze), kiwanda cha NEV kinaweza kuunganisha sehemu zote za gari moja ndani ya saa nne.

Ikiwa ni nchi inayoongoza kwa utengenezaji bidhaa duniani, China ina kategoria pana ya viwanda na mfumo kamili wa usaidizi. Nyenzo na vifaa vingi vinaweza kupatikana kutoka kwa wasambazaji wa ndani, vikisaidia uzalishaji wa majaribio na uzalishaji mkubwa wa bidhaa za uvumbuzi. Kuhusisha nguvu bora ya ushindani na utoaji ruzuku, kunapuuza juhudi zinazofanywa na watu wa China wa kizazi hadi kizazi. 

Nguvu bora ya ushindani inatokana na soko kubwa la China kufunguliwa mlango kwa pande zote.

China imeendeleza siku zote viwanda vya kijani kwa sera ya kufungua mlango, na kuhimiza ushindani. Mwaka 2022, China ilichukua hatua muhimu kwa kuondoa kabisa vizuizi kwa uwekezaji wa kigeni katika sekta ya magari, ikionyesha dhamira yake ya kufungua mlango zaidi kwa dunia nzima.

Watembeleaji wa maonyesho wakitazama onyesho la kituo cha kubadilisha betri cha chapa ya magari ya NIO ya China kwenye Maonyesho ya Kimataifa ya Magari ya Beijing 2024 katika Wilaya ya Shunyi, Beijing, China, Aprili 25, 2024. (Picha: Xinhua)

Watembeleaji wakitazama maonyesho kwenye kituo cha kubadilisha betri cha chapa ya magari ya NIO ya China kwenye Maonyesho ya Kimataifa ya Magari ya Beijing 2024 katika Eneo la Shunyi, Beijing, China, Aprili 25, 2024. (Picha: Xinhua)

China imekumbatia chapa za kigeni kama Tesla na kuhamasisha kampuni mpya za magari, kama vile kampuni za magari za NIO, XPeng na Li, kutumia kikamilifu miundo mipya ya biashara, miundo bunifu ya uendeshaji ya watumiaji na bidhaa za kimapinduzi. Hii imekuza ushindani mzuri kati ya kampuni za ndani na nje ya China za NEVs katika soko la China, huku chapa hizi zikishindana na kuimarishana. Kwa pamoja, zimewapa wanunuzi bidhaa za kiwango cha juu na uzoefu wa kipekee wa watumiaji, na kuongeza ushindani wa jumla wa kampuni zote.

Kuhusisha nguvu bora ya ushindani na ruzuku pia kunapuuza juhudi za kampuni nyingi za nishati mpya za China na nje ya nchi wakati zikijitahidi kupata uungaji mkono wa soko.

Hatimaye, nguvu bora ya ushindani ya China inategemea mwongozo wa kisayansi wa mawazo na dhana mpya.

Chini ya mwongozo wa fikra ya Xi Jinping juu ya uchumi, kampuni za kuzalisha bidhaa za China zimetekeleza kwa uaminifu na kikamilifu dhana mpya za maendeleo. Zimeharakisha uanzishwaji wa muundo mpya wa maendeleo, unaolenga kuhimiza maendeleo yenye sifa bora na kufungamanisha mawazo ya uvumbuzi, uratibu, usio na uchafuzi , uwazi na kunufaisha pamoja na faida katika ugawaji wa raslimali muhimu za uzalishaji na mchakato wa maendeleo ya kiuchumi. Juhudi hizi zimeimarisha kwa kiasi kikubwa ufanisi wa ugawaji wa rasilimali na tija ya jumla ya mambo, kuhimiza mchanganyiko bora wa wafanyakazi wenye sifa bora na wajasiriamali , njia za uzalishaji za teknolojia za akili mnemba na za kidijitali, na kushirikisha vitu vingi zaidi vinavyolengwa na kazi. Kwa hivyo, nguvu bora ya ushindani ya kampuni husika imeendelea kuboreshwa.

Kwa kuongozwa na dhana mpya ya "nguvu mpya za uzalishaji zenye sifa bora," viwanda vya nishati mpya vya China vinafanya juhudi zaidi za kuendana na mwelekeo mkuu wa kubadilisha muundo wa uzalishaji kuwa wa kijani, wenye teknolojia za akili mnemba, na kidijitali kutokana na mapinduzi ya nne ya viwanda. Na vinaharakisha uvumbuzi wa teknolojia za kijani na utumiaji wa teknolojia za kutoa kaboni chache, na kupata mafanikio makubwa katika maendeleo ya kijani.

Ni jambo lisilopingika kwamba China imetekeleza sera kadhaa kuhusu viwanda vya uzalishaji bidhaa ili kuhimiza maendeleo ya uzalishaji usio na uchafuzi. Hata hivyo, sera kama hizo siyo za China pekee .

Makala katika gazeti la South China Morning Post inabainisha kuwa Marekani na EU ni watangulizi na wadau katika kutoa sera ya ruzuku za serikali. Mwaka 2022, serikali ya Marekani ilipitisha Sheria ya Kupunguza Mfumuko wa Bei, ikitoa dola takriban bilioni 369 kama motisha ya ushuru na ruzuku kwa viwanda vikiwemo viwanda vya magari yanayotumia umeme. Nchi kadhaa za Ulaya pia zimetekeleza hatua za ruzuku kwa viwanda vya magari yanayotumia umeme, kuanzia zile za ushuru wa kampuni hadi za manunuzi wa mtu binafsi.

Kama hii ni desturi ya kawaida, kwa nini baadhi ya watu katika nchi fulani mara kwa mara hukosoa sera hizo za China?

Mtazamo wao wa kuumizwa na maendeleo ya China unapaswa kujilaumu wenyewe. China ina nguvu bora kutokana na mfumo wa uchumi wa soko huria wa kijamaa, ukihimiza mwingiliano mzuri kati ya serikali thabiti na soko lenye ufanisi. Mwaka 2009, baada ya msukosuko wa mambo ya fedha wa kimataifa, China ilitoa mpango wa kimkakati wa kuongoza maendeleo ya siku za baadaye, ikipendekeza kuendeleza viwanda kama vile NEV kuwa viwanda vya nguzo na kuanzisha mfululizo wa sera za kuviunga mkono.

Katika muongo mmoja uliopita, hatua madhubuti na sera zenye ufanisi zimeanzisha mazingira mazuri ya maendeleo kwa viwanda vinavyoibuka, na kuvisaidia kustawi. Kwa kuona mafanikio ya China, baadhi ya watu katika nchi fulani huhisi wivu bila shaka na kukimbilia kutumia kisingizio cha ruzuku kukandamiza China.

Shutuma zao zisizo na msingi, zikichochewa na hisia ya kiburi ya umwamba, ni mfano wa wazi wa tabia ya ndumila kuwili. Scott Lincicome, mtaalam wa biashara katika Taasisi ya Cato nchini Marekani, anasema kwa uwazi kwamba shutuma dhidi ya China ni mfano wazi wa kutumia vipimo viwili. Wei Qijia, mtafiti katika Kituo cha Habari cha Serikali ya China, anaamini kwamba wasiwasi huo unatokana na sera zisiyo za sawasawa, na "kujigongana wenyewe" na kutumia “vipimo viwili kwa kawaida, ili kujilinda kibiashara.

Roboti ikifanya kazi kwenye mstari wa kuunda magari wa kampuni ya magari ya FAW-Hongqi huko Changchun, Mkoa wa Jilin, Kaskazini-Mashariki mwa China, Aprili 24, 2024. (Picha: Xinhua)

Roboti ikifanya kazi kwenye mstari wa kuunda magari wa kampuni ya magari ya FAW-Hongqi huko Changchun, Mkoa wa Jilin, Kaskazini-Mashariki mwa China, Aprili 24, 2024. (Picha: Xinhua)

Vitu vyote duniani vimeanzishwa na kustawi kwa kufuata hali halisi, kufeli katika uongo na kuharibiwa kwa udanganyifu. China siku zote imetetea ushirikiano wa uwazi na kunufaishana, kamwe haikimbii ushindani mzuri.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha