Maoni: Kuzidisha ushirikiano na kampuni za China ili kusaidia maendeleo ya NEVs zilizounganishwa teknolojia ya kisasa ya China kufikia kiwango kipya

By Ofisa Mtendaji Mkuu wa Volkswagen (China) Ralf Brandstätter (Tovuti ya Gazeti la Umma) April 28, 2024

Katika miaka ya hivi karibuni, soko la magari yanayotumia nishati mpya (NEVs) la China limepata maendeleo ya haraka. Mwaka 2020 soko lilitabiriwa kuwa magari yanayotumia nishati mpya yatachukua 25% ya jumla ya mauzo ya magari ya China hadi ifikapo Mwaka 2025. Lakini kutokana na hali ya hivi sasa, makadirio hayo yamebadilika, magari hayo sasa yatachukua nusu ya jumla ya mauzo ya magari ya China mwaka mzima 2025, na kiwango hicho kitakuwa cha juu zaidi hadi kufikia 75% mwaka 2030, huku magari yanayotumia umeme pekee yakiwa mtindo mkuu.

Kwa sasa, China inaongoza katika maendeleo ya teknolojia mpya kama vile magari ya kujiendesha yenyenwe bila dereva, sehemu ya dereva yenye teknolojia za kisasa, na huduma ya intaneti kwenye magari huku ikijaa hamasa ya uvumbuzi.

Umri wa wastani wa wamiliki wa magari mapya nchini China ni karibu miaka 35, ambayo ni umri mdogo kwa miaka 20 kuliko wale wa Ulaya. Wamiliki hawa vijana wa magari wana shauku zaidi na wako tayari kujaribu teknolojia za kisasa za akili mnemba na za kidijitali.

Ukitazama kote duniani, hakuna nchi yoyote ambayo tasnia yake ya magari inaweza kushindana na ile ya China katika mageuzi na uvumbuzi wa kasi. Hakuna shaka kwamba mustakabali wa baadaye ni wa magari yanayotumia nishati mpya na magari yaliyounganishwa na teknolojia za akili mnema, na China imekuwa soko lililoendelea zaidi duniani la magari hayo.

Kwa watengenezaji magari wa kimataifa, maendeleo ya haraka ya sekta ya magari ya China yameleta changamoto, lakini mambo muhimu zaidi yaliyoyaleta ni fursa. Watengenezaji wa kimataifa wenye uzoefu mkubwa wana uwezo bora wa R&D (Utafiti na Maendeleo) wa magari na teknolojia za uhandisi za magari, ambao unaongoza katika tasnia. Hata hivyo, kampuni za teknolojia za China zinaendelea kupata mafanikio mapya katika nyanja ya teknolojia ya kisasa ya magari yanayotumia umeme kwa kuzingatia mahitaji ya kipekee ya soko la China.

Katika zama mpya, kujenga muundo mpya wa ushirikiano wa uvumbuzi kati ya China na nchi nyingine na kuchanganya faida na rasilimali za kila mmoja kutanufaisha pande zote na kuhimiza zaidi maendeleo yenye ubora wa hali ya juu ya viwanda vya magari yanayotumia nishati mpya vya China.

Katika kipindi cha miaka 40 iliyopita kundi la kampuni za Volkswagen likiwa limejitahidi kujiendeleza katika soko la China, likitafuta kwa uendelevu miundo bunifu ya ushirikiano na viwanda vya magari ya China. Hii pia ni kipaumbele cha juu cha kazi yake ya sasa.

Mwanzoni mwa mwaka huu, kundi hilo la kampuni liliwekeza Euro bilioni 1 na kuanzisha Kampuni ya Teknolojia ya Volkswagen (China) huko Hefei, Mkoa wa Anhui, ambayo imeanza kufanya kazi rasmi. Hiki ni kituo kikubwa zaidi cha R&D nje ya makao makuu ya kundi hilo huko Ujerumani. Kinajikita katika R&D, mambo ya uvumbuzi na ununuzi wa magari yanayotumia umeme na kuunganishwa teknolojia za kisasa, kikiwa ni kiunganishi muhimu cha kundi hilo na washirika wake wa China. Kituo hicho kinaliwezesha kundi hilo kufanya maamuzi ya haraka kulingana na hali halisi ya soko la China, na kufanya utambuzi wa sehemu za magari na teknolojia zao nchini China, hivyo kufupisha kwa 30% mchakato wa maendelo ya bidhaa mpya na teknolojia mpya, na kuliwezesha kundi hilo kufungamanishwa vizuri katika mfumo wa teknolojia wa China.

Hivi karibuni, Kundi la Kampuni za Volkswagen lilitangaza uwekezaji mwingine wenye thamani ya euro zaidi ya bilioni 2.5 nchini China ili kupanua zaidi kituo chake cha uzalishaji na uvumbuzi mjini Hefei. Azma yake ya kufungamana na soko la China na kuimarisha uwezo wake wa R&D nchini China inadhihirisha sana.

Zaidi, kupitia ushirikiano wa kimkakati na kampuni ya magari yanayotumia nishati mpya ya Xpeng Motors ya China, kampuni hizo mbili si tu zitaunda modeli mbili za NEVs yanayotumia teknolojia ya kisasa yenye ukubwa wa kati, bali pia zitaendeleza kwa pamoja usanifu ongozi wa kielektroniki unaoitwa CEA, hivyo kuendelea kuwapa wateja huduma za kisasa zaidi za kidijitali na zenye akili zaidi.

Katika nyanja za magari ya kujiendesha yenyewe, mifumo ya habari-burudani, betri za nishati na kadhalika, Kundi la Volkswagen limeshirikiana na kampuni za teknolojia za China kama vile Horizon, Chuangda, na Guoxuan, na linaendelea kutafuta na kuzidisha ushirikiano wa uvumbuzi na kampuni tatu zenye ubia mkubwa zaidi za magari nchini China katika maendeleo ya magari yanayotumia nishati mpya.

Ushirikiano unahimiza maendeleo ya kiteknolojia na ustawi wa viwanda. Tunatekeleza kwa uthabiti mkakati wa maendeleo wa "nchini China, kwa China" na kufanya kazi bega kwa bega na wenzetu wa China. Tunaamini kwamba kwa pande zote husika kujumuisha juhudi na kuunganisha rasilimali na manufaa katika kamba moja, tutaweza kukumbatia vizuri zaidi mageuzi ya magari ya teknolojia za akili mnemba katika siku za baadaye na kusaidia tasnia ya magari ya China kuunda nafasi pana kwa maendeleo.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha