Waziri wa Usalama wa Umma wa China akutana na waziri wa mambo ya ndani wa Cape Verde

(Tovuti ya Gazeti la Umma) April 29, 2024

Waziri wa Usalama wa Umma wa China, Wang Xiaohong akikutana na Paulo Rocha, Waziri wa Mambo ya Ndani wa Cape Verde, mjini Beijing, China, Aprili 26, 2024. (Xinhua/Yin Bogu)

Waziri wa Usalama wa Umma wa China, Wang Xiaohong akikutana na Paulo Rocha, Waziri wa Mambo ya Ndani wa Cape Verde, mjini Beijing, China, Aprili 26, 2024. (Xinhua/Yin Bogu)

BEIJING - Waziri wa Usalama wa Umma wa China, Wang Xiaohong amekutana na Paulo Rocha, Waziri wa Mambo ya Ndani wa Cape Verde, siku ya Ijumaa mjini Beijing, akisema kuwa chini ya mwongozo wa kimkakati wa viongozi wa nchi hizo mbili, uhusiano wa pande mbili unaendelea vizuri huku kukiwa na ushirikiano wenye matunda halisi katika sekta mbalimbali.

Wang amesema, China ingependa kushirikiana na Cape Verde katika kuimarisha ushirikiano wa utekelezaji wa sheria kwenye ngazi zote, kuimarisha ushirikiano wa usalama wa Ukanda Mmoja, Njia Moja, kupambana na uhalifu wa kuvuka mipaka, na kulinda usalama wa raia, taasisi na miradi ya kila upande wa nchi hizo mbili.

“China ingependa kulinda maslahi ya pamoja ya nchi hizo mbili, na kuhimiza uhusiano kati ya China na Cape Verde, China na Afrika uendelee kwenye ngazi mpya”, amesema Wang.

Paulo Rocha amesema Cape Verde ingependa kuzidisha zaidi ushirikiano na China katika utekelezaji wa sheria na usalama.

Waziri wa Usalama wa Umma wa China, Wang Xiaohong akikutana na Paulo Rocha, Waziri wa Mambo ya Ndani wa Cape Verde, mjini Beijing, China, Aprili 26, 2024. (Xinhua/Yin Bogu)

Waziri wa Usalama wa Umma wa China, Wang Xiaohong akikutana na Paulo Rocha, Waziri wa Mambo ya Ndani wa Cape Verde, mjini Beijing, China, Aprili 26, 2024. (Xinhua/Yin Bogu)

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Renato Lu)

Picha