Waziri Mkuu wa China asema soko la China linafungua mlango wake muda wote kwa kampuni za kigeni

(Tovuti ya Gazeti la Umma) April 29, 2024

Waziri Mkuu wa China Li Qiang akikutana na Elon Musk, Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya magari yanayotumia umeme ya Marekani ya Tesla, mjini Beijing, China, Aprili 28, 2024. (Xinhua/Wang Ye)

Waziri Mkuu wa China Li Qiang akikutana na Elon Musk, Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya magari yanayotumia umeme ya Marekani ya Tesla, mjini Beijing, China, Aprili 28, 2024. (Xinhua/Wang Ye)

Beijing - Waziri Mkuu wa China Li Qiang amekutana na Elon Musk, Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya magari yanayotumia umeme ya Marekani ya Tesla, mjini Beijing siku ya Jumapili, na kuahidi kuwa soko la China siku zote litafungua mlango wake kwa kampuni zinazowekezwa kwa mtaji wa kigeni.

Akiyaelezea maendeleo ya Tesla nchini China kuwa mfano mzuri wa ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara kati ya China na Marekani, Waziri Mkuu Li amesema ukweli umethibitisha kwamba ushirikiano wa usawa na kunufaishana unatumikia maslahi ya kimsingi ya nchi zote mbili, na unaendana na matarajio ya pamoja ya watu wa pande hizo mbili.

“Inatarajiwa kuwa Marekani itashirikiana zaidi na China kufuata mwongozo wa kimkakati wa wakuu wa nchi hizo mbili na kuhimiza uhusiano kati ya pande mbili kuendelea kuendelezwa kwa utulivu, na kunufaisha zaidi watu wa nchi hizo mbili na kwa dunia nzima” Waziri Mkuu Li amesema.

Huku akibainisha kuwa kampuni zinazowekezwa kwa mtaji wa kigeni ni washiriki na watoaji mchango muhimu katika maendeleo ya China, Waziri Mkuu Li amesema kuwa soko kubwa la China siku zote litafungua mlango.

Amesema, China itachukua hatua zinazoendana na maneno yake na kuongeza juhudi zake katika kupanua upatikanaji wa soko na kuimarisha huduma, miongoni mwa maeneo mengine, ili kutoa mazingira mazuri zaidi ya kibiashara na uungaji mkono zaidi kwa kampuni za kigeni.

Kwa upande wake Musk amesema kuwa kiwanda cha Shanghai cha Tesla ndicho kiwanda kinachofanya kazi vizuri zaidi cha kampuni hiyo, kutokana na bidii na hekima za timu yake ya China, na Tesla ingependa kuzidisha ushirikiano na China ili kupata matokeo mengi zaidi ya kunufaishana.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Renato Lu)

Picha