Mkutano maalum wa Baraza la Uchumi Duniani waanza mjini Riyadh, Saudi Arabia

(Tovuti ya Gazeti la Umma) April 29, 2024

Mkutano maalum wa Baraza la Uchumi Duniani (WEF) ukianza mjini Riyadh, Saudi Arabia, Aprili 28, 2024. (Xinhua/Wang Haizhou)

Mkutano maalum wa Baraza la Uchumi Duniani (WEF) ukianza mjini Riyadh, Saudi Arabia, Aprili 28, 2024. (Xinhua/Wang Haizhou)

RIYADH - Mkutano maalum wa Baraza la Uchumi Duniani (WEF) umeanza jana siku ya Jumapili mjini Riyadh, Saudi Arabia ukilenga ushirikiano wa kimataifa, ukuaji wa uchumi na nishati kwa ajili ya maendeleo.

"Leo, tunakusanyika katika wakati ambapo dunia inakabiliwa na mabadiliko mengi, huku uchumi, jamii, na sekta ya viwanda vyetu vikikabiliwa na changamoto zisizo na kifani na fursa kubwa," Waziri wa Uchumi na Mipango wa Saudi Arabia, Faisal bin Fadhil Alibrahim amesema kwenye hafla ya ufunguzi wa mkutano huo maalum, akisisitiza umuhimu wa ushiriki duniani kwa uchumi wa dunia unaonufaisha kila mtu.

Rais wa WEF Borge Brende amesema mkutano huo ni tukio muhimu la kupitia maendeleo yaliyopatikana katika kupunguza migogoro katika eneo la Mashariki ya Kati, hali ya kibinadamu huko Gaza na mada nyingine muhimu za kikanda na za kimataifa.

Mkutano huo wa WEF utaendelea hadi Jumatatu wiki ijayo, kwa lengo la kuwezesha mazungumzo kati ya wanaoongoza mawazo na umma kuhusu mada mbalimbali zikiwemo changamoto za mazingira, afya ya akili, sarafu za kidijitali, akili bandia, mchango wa sanaa katika jamii, ujasiriamali wa kisasa, na miji ya kisasa.

Rais wa Baraza la Uchumi Duniani (WEF) Borge Brende akizungumza kwenye hafla ya ufunguzi wa mkutano maalum wa WEF, unaofanyika Riyadh, Saudi Arabia, Aprili 28, 2024. (Xinhua/Wang Haizhou)

Rais wa Baraza la Uchumi Duniani (WEF) Borge Brende akizungumza kwenye hafla ya ufunguzi wa mkutano maalum wa WEF, unaofanyika Riyadh, Saudi Arabia, Aprili 28, 2024. (Xinhua/Wang Haizhou)

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Renato Lu)

Picha