Israel kutuma ujumbe nchini Misri kushiriki kwenye mazungumzo ya kusimamisha vita

(Tovuti ya Gazeti la Umma) April 30, 2024

Ofisa wa serikali ya Israel aliwathibitishia waandishi wa habari wa Shirika la Habari la China, Xinhua tarehe 29 kwamba Israel itatuma ujumbe nchini Misri tarehe 30 kushiriki katika mazungumzo ya kusitisha mapigano na Palestina.

Habari nyingine kutoka Shirika la Utangazaji la Israel(IBA) tarehe 29 zinasema, wawakilishi wa Hamas wamefika Misri siku hiyo. Habari zinasema, Israel imekubali kuwa, ikiwa Hamas itawaachilia huru Waisraeli 33 waliofungwa, Israel itaachiliwa huru maelfu ya Wapalestina waliokuwa wamefungwa.

Kundi la Hamas lilitoa taarifa alfajiri ya tarehe 27, ikisema kuwa kundi hilo limepata sharti la Israel kwenye makubaliano ya kusitisha mapigano katika Ukanda wa Gaza na kwa sasa inafanya uchunguzi kuhusu hilo. Habari kutoka Channel 12 ya Kituo cha Televisheni cha Israel zinasema, ujumbe wa Misri ulifanya mazungumzo na ujumbe wa Israel tarehe 26, ambapo Israel imewasilisha masharti yake kwenye makubaliano ya kusitisha mapigano kwa Hamas kupitia Misri, na kusema kuwa hiyo itakuwa fursa ya mwisho ya kufikia makubaliano kabla ya jeshi la Israel kufanya shambulio katika Rafah, kusini mwa Ukanda wa Gaza.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha