Mafunzo mfululizo ya kikamilifu yaliyotolewa na kampuni ya China yasaidia kuongeza uwezo wa vipaji wa Waganda

(Tovuti ya Gazeti la Umma) April 30, 2024

Tarehe 27, Aprili, 2024,  wanafunzi  wakifanya mazoezi ya kufunga rebar chini ya mafunzo ya mhandisi wa China mjini Kampala, Uganda. (Picha na Hajarah Nalwadda/Xinhua)

Tarehe 27, Aprili, 2024, wanafunzi wakifanya mazoezi ya kufunga rebar chini ya mafunzo ya mhandisi wa China mjini Kampala, Uganda. (Picha na Hajarah Nalwadda/Xinhua)

Kampuni za China zinashiriki kwenye maendeleo ya uchumi wa Uganda na kutoa mafunzo ya kazi ya ufundi na ujuzi wa kitaalamu kwa wafanyakazi huko.

Musitwa Abel ni mmoja kati ya wafanyakazi 32 Waganda wa Kampuni ya Ujenzi na Mawasiliano ya China (CCCC) tawi la Uganda, ambao wamemaliza masomo yao ya wiki mbili kwenye mafunzo yaliyotolewa na kampuni hiyo kwa kushirikiana na Chuo cha Kazi ya Ufundi cha Mji cha Wuhan (WCP).

Mafunzo hayo ni sehemu moja ya mradi wa kampuni hiyo wa kuwaandaa vipaji wenyeji, “Mradi wa Seagull”, ambao unahusisha mafunzo ya kinadharia na ya mazoezi yakiwemo uchoraji wa ramani ya uhandisi, mashine za uhandisi, na matumizi ya lugha ya Kichina.

Katika muongo mmoja uliopita, Abel alipandishwa cheo chake kutoka dereva wa kusafirisha raslimali za ujenzi wa majengo hadi kuwa fundi wa maabara. Hivi sasa hata anasomea shahada ya uhandisi wa programu ya kompyuta katika chuo kikuu cha uwazi.

Katika mahojiano ya hivi karibuni Abel aliambia Shirika la Habari la China Xinhua kuwa, “Tangu nilipojiunga na kampuni ya CCCC, hali yangu ya kiuchumi imeboreshwa hatua kwa hatua. Ufundi na ujuzi wa sekta mbalimbali niliopata kutoka kwenye kampuni ya CCCC unanisaidia sana kufanya kazi vizuri.”

Mwakilishi wa kampuni ya CCCC tawi la Uganda Zhao Wei alisema, mafunzo ya aina hayo ni muhmu sana, kwa sababu kampuni hiyo inazingatia namna ya kuwezesha maendeleo endelevu nchini humo.

Zhao alisema, maelfu ya wafanyakazi wenyeji, wakiwemo pamoja na wataalamu wa rasilimali watu, wahandisi wa kutathmini mazingira, wahandisi wa usalama, wasimamizi wa kazi na waendeshaji wa mashine, wote wameshiriki kwenye ujenzi wa miradi ya kampuni hiyo nchini Uganda.

Tarehe 27, Aprili, 2024,  watu walioshiriki kwenye “Mradi wa Seagull” wakiwa kwenye darasa la nadharia ya ujenzi huko Wakiso, Uganda. (Picha na Hajarah Nalwadda/Xinhua)

Tarehe 27, Aprili, 2024, watu walioshiriki kwenye “Mradi wa Seagull” wakiwa kwenye darasa la nadharia ya ujenzi huko Wakiso, Uganda. (Picha na Hajarah Nalwadda/Xinhua)

Tarehe 27, Aprili, 2024, mwalimu wa lugha ya Kichina Zhou Chuan  akifundisha darasa la lugha ya Kichina huko Wakiso, Uganda. (Picha na Hajarah Nalwadda/Xinhua)

Tarehe 27, Aprili, 2024, mwalimu wa lugha ya Kichina Zhou Chuan akifundisha darasa la lugha ya Kichina huko Wakiso, Uganda. (Picha na Hajarah Nalwadda/Xinhua)

Tarehe 27, Aprili, 2024, mfanyakazi wa kampuni ya CCCC Musitwa Abel ambaye alimaliza masomo kwenye mafunzo ya wiki mbili ya “Mradi wa Seagull” alihojiwa huko Kampala, Uganda. (Picha na Hajarah Nalwadda/Xinhua)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha