Rais Xi Jinping ajibu barua kutoka kwa wafanyakazi wa kiwanda cha chuma cha Serbia

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Mei 02, 2024

BEIJING - Rais Xi Jinping wa China amejibu barua kutoka kwa wafanyakazi wa Serbia wa Kiwanda cha Chuma cha HBIS Smederevo ambapo kwenye barua hiyo, amewahamasisha wafanyakazi hao kutoa mchango mpya kwenye urafiki kati ya China na Serbia.

Rais Xi amesema kwenye ziara yake nchini Serbia Mwaka 2016, alikutana na wafanyakazi hao uso kwa uso kwenye kiwanda hicho na kuguswa sana na uungaji mkono wao kwa ushirikiano wa kunufaishana kati ya China na Serbia, na matarajio yao makubwa kwa mustakabali mzuri wa kiwanda hicho cha chuma.

Kutoka kwenye barua yao hiyo, Rais Xi amefahamu kwamba kutokana na juhudi za pamoja za timu za usimamizi za pande zote mbili na wafanyakazi wenyewe, kiwanda hicho cha chuma kimepata sura mpya, kikitoa uungaji mkono mkubwa kwa maendeleo ya Mji wa Smederevo.

“Ni furaha kubwa sana kujua kwamba kiwanda hicho cha chuma kimepata faida kwa kasi baada ya kampuni moja ya China kuwezaka, huku ajira za watu zaidi ya 5,000 zikiwa zimehakikishwa, na maelfu ya familia zikifurahia maisha ya amani na furaha” amesema rais Xi.

Amesema, maendeleo ya kiwanda hicho, hayawezi kupatikana bila kujitolea na kufanya kazi kwa bidii kwa wafanyakazi, ambao wamekuwa wakifanya kazi bila kuchoka kwa ajili ya ukuaji wa kasi wa kiwanda hicho na wameandika ukurasa mpya kwa urafiki imara kama chuma kati ya China na Serbia.

"Ninawapa 'ishara ya dole gumba',” Rais Xi amesema.

Maendeleo mazuri ya kiwanda hicho ni ushahidi mkubwa wa ushirikiano wa kiwango cha juu wa Ukanda Mmoja, Njia Moja kati ya China na Serbia, vilevile mfano mzuri wa ushirikiano wao wa kunufaishana, amesema, huku akiongeza kuwa wafanyakazi wa kiwanda hicho cha chuma ni washiriki, mashuhuda, watoaji mchango na wanufaika wa ushirikiano wa kirafiki kati ya China na Serbia.

“Natumai mtaendelea kufanya kazi zenu wenyewe kwa moyo wote na kujitolea kwa hamasa kwenye uendeshaji na maendeleo ya kiwanda hicho, ili kutoa mchango mpya na mkubwa zaidi kwenye maendeleo ya kijamii na kiuchumi ya Serbia na kuimarisha urafiki kati ya China na Serbia.

Wawakilishi kumi na tatu wa kiwanda hicho, walimwandikia barua Rais Xi, wakielezea kuhusu maendeleo mapya ya kiwanda hicho na mchango wake muhimu katika kuboresha ustawi wa wenyeji. Katika barua hiyo pia wamemshukuru Rais Xi kwa kujali na kuwezesha mradi huo.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha