Kitabu chenye thamani zaidi cha Confucius chaonesha mawasiliano ya kitamaduni kati ya China na Ufaransa

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Mei 05, 2024

Rais wa China Xi Jinping atafanya ziara ya kiserikali nchini Ufaransa kutokana na mwaliko wa Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa.

Wakati wa ziara ya kiserikali ya Rais Xi nchini Ufaransa miaka mitano iliyopita, Macron alimpa zawadi ya toleo la Kifaransa la kitabu cha "Confucius, au Sayansi ya Princes." Macron alieleza kuwa Fikra ya wasomi wa Confucius iliwapa ufunuo wanafikra Wafaransa kama vile Voltaire na kuchochea sana uvuguvugu wa uelewa wa Ufaransa.

Kitabu hicho kinajumuisha fikra iliyotukuka ya wasomi wa Confucius, fikra hiyo ambayo imevuka nyakati na nafasi. Kinatumika kama ushuhuda wa simulizi ya kuthaminiana na kufundishana kati ya China na Ufaransa, nchi mbili muhimu wakilishi wa ustaarabu wa Mashariki na Magharibi.

Kadiri ziara na mawasiliano vinavyoongezeka, ndivyo ukunjufu na ukaribu unavyoongezeka kati ya nchi hizo mbili. Ziara hiyo ya Rais Xi nchini Ufaransa inatarajiwa kufungua ukurasa mpya wa uhusiano kati ya China na Ufaransa na kuongeza msukumo wa kubadilishana mawazo na kufundishana kati ya nchi hizo mbili.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha