Halo Kite!

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Mei 05, 2024

Mwaka 1958, filamu ya "Maajabu ya Tiara," ilianza kuoneshwa kwenye majumba ya sinema ya Ufaransa, filamu ambayo ni ya kwanza iliyopigwa kwa pamoja na Jamhuri ya Watu wa China na nchi ya kigeni. Katika filamu hiyo, Tiara ya ajabu ilibuniwa kutokana na mhusika Sun Wukong ambaye ni Mfalme Kima katika filamu ya China, na Tiara hiyo ilijenga urafiki kati ya watoto wa China na Ufaransa. Mwaka huu ni maadhimisho ya miaka 60 tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia kati ya China na Ufaransa. Tiara hiyo ya alama imesafiri kwa anga, ikipaa kutoka nchi moja hadi nchi nyingine, ikiwa imebeba urafiki na matumaini kutoka siku zilizopita hadi siku za baadaye. Kusafiri kwake angani kumetunga simulizi ya kudumu ya uhusiano wa karibu kati ya nchi hizo mbili, na uhusiano huo hata milima mikubwa na mito haiwezi kuutenganisha.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha