“Sisi ni Marafiki”: Urafiki wa China na Serbia waimarika kwa kupitia Katuni

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Mei 07, 2024

Hivi karibuni, shughuli ya kuonesha filamu za katuni za Serbia ilifanyika katika Kituo cha Mawasiliano ya Kitamaduni cha Serbia hapa Beijing, ambapo filamu hizi bunifu zilipigiwa makofi ya furaha na watazamaji.

Wajumbe wa Chuo cha Filamu ya Katuni cha Vranje cha Serbia wameleta filamu 10 za katuni zenye maudhui tofauti na mitindo tofauti kuja kuzionesha nchini China, ambapo wamejadiliana na wadau wa nyanja za filamu za katuni za China na watazamaji wa China.

Mwalimu mkuu wa Chuo cha Filamu ya Katuni cha Vranje cha Serbia Jasmina Stojanovic alipohojiwa na People’s Daily Online alijulisha kuwa, chuo hicho kilianzishwa miaka ya 1980 na kinajikita katika mpango wa kuwawezesha watoto wote na vijana wote kuwa na usawa wa kubuni sanaa ya katuni. Baada ya maendeleo ya miaka mingi, chuo hicho kimekuwa ofisi ya kiumma ya serikali ya Serbia kutoka shirika la jamii ya awali.

“Hii ni mara yangu ya kwanza kuja China. Safari hiyo imenipa picha nzuri,” alisema Stojanovic, akiongeza kuwa, mawasiliano katika utamaduni na sanaa yanasaidia kuimarisha urafiki, na anatumai kwa kupitia shughuli hiyo wataweza kuwaelezea watazamaji wa China simulizi za Serbia, na kuongeza hali ya kufahamiana na kuelewana kati ya watu wa nchi hizo mbili.

“Natumai kwa kupitia safari hiyo katika China nitaweza kuwasiliana na wadau wa nyanja za filamu za katuni wa China kuhusu uzoefu, na kujadiliana nao kuhusu maswali,” alisema mwalimu wa Chuo cha Filamu ya Katuni cha Vranje cha Serbia SneZana Trajkovic alipohojiwa. “Marafiki zangu wengi wanavutiwa na kuja China kufanya mawasiliano. Na pia ninatarajia siku za baadaye marafiki wengi zaidi wa China watakwenda Serbia kufanya mawasiliano.”

“Haya ni mawasiliano yanayoongeza hamasa,” alisema Wandao, mwanafunzi wa Chuo cha Katuni na Sanaa ya Kidijitali katika Chuo Kikuu cha Mawasiliano ya Habari cha China. Anatumai shughuli kama hiyo zitaingia chuoni na wahusika wa pande mbili watashirikiana zaidi ili kubuni sanaa nyingi zinazoonesha umaalumu na sifa pekee za mataifa mawili.

Katika miaka ya hivi karibuni, shughuli za mawasiliano ya utamaduni kati ya China na Serbia zimeongezeka zaidi, na zinahimiza maelewano kati ya watu wa nchi mbili. Mtazamaji aliyeshiriki kwenye shughuli hiyo Guo Kun alipanga kutembelea Serbia pamoja na watoto wake, na baada ya shughuli hiyo, alivutiwa zaidi na utamaduni wa Serbia. “Natumai kutakuwa na shughuli nyingi zaidi kama hiyo ya leo, na kuwafahamisha Wachina wengi zaidi kuhusu Serbia,” alisema Guo Kun, na “ watu wa nchi zetu mbili watakuwa kama marafaiki wa karibu zaidi siku hadi siku.”

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Renato Lu)

Picha