Mwanafunzi wa Serbia: Ninatarajia kuwa na muunganisho zaidi na China

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Mei 07, 2024

"Nataka kujua kwa nini China ina uwezo mkubwa namna hii katika karne ya 21?” Yovana Marsenic, ambaye ni mwanafunzi kutoka Serbia anayesoma kozi ya siasa ya kimataifa katika Chuo Kikuu cha Pili cha Lugha za Kigeni cha Beijing alisema wakati anapoulizwa sababu ya kuja China kujifunza lugha ya Kichina,.

Mnamo mwaka 2019, Yovana alipata fursa ya kujifunza kwenye Chuo Kikuu cha Jiaotong cha Xi'an. Ikiwa ni safari yake ya kwanza nchini China, Yovana alitembelea vivutio vingi vya kitalii kama vile Makaburi ya Mfalme mwanzilishi wa Qin, na "Mtaa wa Datang". Amesema, “China ni nchi yenye historia ndefu na utamaduni wa kuvutia, hata siishiwi hamu ya kuangalia!”

Yovana siyo tu alitembelea vivutio vya mabaki ya kale, bali pia amepata uzoefu wa ukarimu wa wenyeji katika mitaa yanayoonesha hamasa ya maisha, na kuonja vyakula vitamu vya China. Yovana alisema, “Tabia za Wachina na Waserbia kuhusu vyakula ni tofauti, lakini ninapenda vyakula vya China, kama vile jiaozi, bata choma n.k.”

Ingawa aliishi China kwa mwezi tu, siku hizi zilipanda “mbegu” moyoni mwa Yovana. Baada ya kupata shahada yake ya uzamili, alikwenda tena nchini China na kuamua kupata uzoefu kwa kina wa kuelewa maisha ya wenyeji.

Baada ya kuja hapa Beijing mwaka jana, Yovana alitembelea vivutio vya Uwanja wa Tian’anmen, Kasri la Ufalme, Kasri la kale la Kifalme, na Ukuta Mkuu. Katika maisha yake ya kila siku, Yovana hutembelea katika Hutong mjini Beijing, na kuhisi utamaduni wa Bejing. Amesema kuwa, “Ninapenda sana Hutong, kwa sababu inaniwezesha kuhisi utamaduni wa jadi wa China, na kupata fursa ya kuwasiliana na wenyeji na kula chakula kitamu. Naona mambo hayo yananivutia na kunifurahisha sana.”

Akipata fursa ya kujiunga moja kwa moja kwenye jamii ya China, Yovana ameelewa kwa kina zaidi utamaduni wa China. “Maneno ya lugha ya Kichina ni sehemu muhimu ya utamaduni wa China. Wakati ninapojifunza, ninaweza kuelewa namna ya kufikiria ya Wachina, na kuelewa hamasa zao kwa maisha.”

Katika miezi hii alipoishi nchini China, siyo tu Yovana amepata maendeleo makubwa katika lugha ya Kichina, bali pia ameelewa zaidi maisha ya hapa. “Nimegundua kuwa maisha hapa ni ya haraka haraka, miji inaendelea kwa kasi, na utamaduni na teknolojia vinabadilika sana,” alisema Yovana, “naona Beijing ina historia ndefu na tamaduni mbalimbali, na pia ni mji jumuishi ambao uko wazi kwa mawazo mbalimbali na maoni mbalimbali.”

Kwa mtazamo wa Yovana, njia ya kulipia kwa simu nchini China imeleta urahisi mkubwa kwa maisha yake. Ukienda nje, chukua simu na betri tu, haina haja ya kubeba pochi. Yovana amesema chombo cha usafiri anachokipenda zaidi ni sabwei, au treni chini ya ardhi, “ninapokwenda nje pamoja na marafiki zangu ninapenda kupanda sabwei, kwa sababu sabwei ya China ni rahisi kupanda na ni ya kasi, sina wasiwasi ya kuwa na msongamano barabarani na kuchelewa.”

Siku hizi za kuishi nchini China zimemfanya Yovana aimarishe nia yake, ameamua kuendelea kukaa hapa. Kwa upande mmoja anataka kusoma zaidi, kushughulikia kazi husika siku za baadaye na kuwa balozi wa utamaduni kati ya China na Serbia; Kwa upande mwingine, anataka kuelewa zaidi kuhusu utamaduni, lugha na namna ya kufikiri ya Wachina. “Ukitaka kuelewa nchi yenye historia ya zaidi ya miaka 5,000, bila shaka kuishi kwa mwaka mmoja hautoshi,” alisema Yovana.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Renato Lu)

Picha