Lugha yajenga daraja: Vijana wa China na Hungary warithisha urafiki kati ya nchi zao

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Mei 09, 2024

Tihanyi Istvan kutoka Hungary ni mwanzilishi wa duka la mvinyo na kahawa lililopo kwenye eneo la Heping la Mji wa Tianjin, China. Mhitimu huyu wa Chuo Kikuu cha Tianjin licha ya kuendesha duka lake, anasimamia kampuni ya uagizaji na uuzaji bidhaa.

Tihanyi ameishi hapa China kwa zaidi ya muongo mmoja, mke wake ni mwenyeji wa Tianjin, na amezoea maisha nchini China, hata anajua kuongea kwa lafudhi ya Tianjin. Tihanyi alisema, “baada ya kujua mimi ni Mhungary, Hungary ipo wapi, na Hungary ni nchi yenye hali ya namna gani, watu hufurahi sana, wanaweza kusema ‘Hungary ni nchi nzuri na watu wake ni wazuri.’ Ninafurahia maneno waliyosema ya kusifu kama hayo.”

Alipozungumzia kazi na maisha yake ya siku za baadaye, Tihanyi alisema,“Ninatumai nitakuwa balozi wa mawasiliano kati ya nchi hizo mbili, na pia kutumai kuwasaidia Wachina kuijua zaidi Hungary.”

Katika Chuo Kikuu cha Pili cha Lugha za Kigeni cha Beijing kwenye umbali wa zaidi ya kilomita 100 kutoka Tihanyi, kuna vijana wengine wanaofanya juhudi kwa ajili ya urafiki kati ya China na Hungary.

Duan Shuangxi ni mwalimu wa lugha ya Kihungary wa chuo kikuu hicho, na aliwahi kuishi Budapest kwa miaka minane. Katika mafunzo ya darasa lake, Duan anawafundisha wanafunzi lugha ya Kihungary kwa kupitia kusoma habari na kuelezea uhusiano wa China na Hungary. Amesema, lugha ya Kihungary ni ngumu kujifunza lakini inavutia sana.

Akiwa mmoja kati ya wanaohimiza mawasiliano kati ya China na Hungary, Duan amesema, “ kadiri uhusiano wa China na Hungary unavyoendelea, na pendekezo la ‘Ukanda Mmoja, Njia Moja’ linavyoenea duniani, ndivyo kampuni nyingi zaidi za China zinawekeza katika Hungary kwa hivi sasa, na uhusiano huo unaendelea kwa kasi. Katika mwelekeo huo kuna mahitaji mkubwa kwa vipaji wanaojua zaidi lugha ya Kihungary na hali ya nchi hiyo.”

Mpaka sasa Duan amewafundisha wanafunzi zaidi ya 120 waliochukua kozi ya lugha ya Kihungary, na Nie Yuan ndiye mmoja kati ya wanafunzi hao. Nie amesema, “Ninavutiwa sana na Hungary. Natumai kwa kupitia kujifunza lugha yake, siku za baadaye nitapata fursa ya kwenda huko kuwatembelea watu na kujihisi utamaduni wa nchi hiyo. Ninatumai mimi siyo tu nitakuwa mshiriki wa mawasiliano ya kitamaduni kati ya China na nchi za nje, bali pia nitakuwa daraja la kuhimiza mawasiliano ya China na Huagary.”

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Renato Lu)

Picha