Mradi wa uzalishaji wa umeme kwa nishati ya jua unaojengwa na kampuni ya China wazinduliwa Tunisia

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Mei 10, 2024

Uzinduzi wa ujenzi wa kituo cha kuzalisha umeme kwa nishati ya jua cha Kairouan kinachojengwa na Kampuni ya China, ambacho uwezo wake wa uzalishaji ni megawati 100 umefanyika katika Jimbo la Kairouan, Tunisia. Huo ni mradi mkubwa zaidi unaojengwa sasa nchini Tunisia.

Picha hii inaonyesha hali ya uzinduzi wa ujenzi wa Kituo cha kuzalisha umeme kwa nishati ya jua katika Jimbo la Kairouan, nchini Tunisia, Mei 8. (Mpiga picha: Adel Ezzine/Xinhua)

Picha hii inaonyesha hali ya uzinduzi wa ujenzi wa Kituo cha kuzalisha umeme kwa nishati ya jua katika Jimbo la Kairouan, nchini Tunisia, Mei 8. (Mpiga picha: Adel Ezzine/Xinhua)

Wael Chouchane, Katibu ya taifa ya Tunisia anayeshughulikia mambo ya mageuzi ya nishati, aliwaambia waandishi wa habari katika uzinduzi huo kwamba kuanzishwa kwa ujenzi wa mradi huo ni hatua muhimu katika mkakati wa Tunisia wa kukuza nishati ya aina mbalimbali na kutimiza mpito wa nishati.

Meneja wa mradi kutoka Taasisi ya mpango wa Nishati ya Umeme ya Kaskazini Magharibi ya China(NWEPDI),Wang Wenhai alisema kuwa mradi huo unaweza kufanya kazi kwa miaka 25 na kuzalisha umeme wa kilowati saa bilioni 5.5.

Mei 8, wafanyakazi wawili wakionyesha namna ya kuweka paneli za umeme wa nishati ya jua katika Jimbo la Kairouan,nchini Tunisia. (Mpiga picha: Adel Ezzine/Xinhua)

Mei 8, wafanyakazi wawili wakionyesha namna ya kuweka paneli za umeme wa nishati ya jua katika Jimbo la Kairouan,nchini Tunisia. (Mpiga picha: Adel Ezzine/Xinhua)

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Renato Lu)

Picha