Wanafunzi wa shule za msingi nchini Tanzania washiriki kwenye mashindano ya lugha ya Kichina na utamaduni wa China

(CRI Online) Mei 11, 2024

Wanafunzi 14 kutoka shule sita za msingi za nchini Tanzania Jumatano walishiriki kwenye shindano la “Daraja la Lugha ya Kichina” kwa ajili ya wanafunzi wa shule za msingi, ambako walionyesha uwezo wao kuzungumza lugha na ujuzi wao kuhusu utamaduni wa China.

Mashindano hayo yalifanyika katika Chuo cha Confucius cha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Tausi Julius mwenye umri wa miaka kumi kutoka Shule ya Msingi ya Longquan Bodhi iliyoko pembezoni mwa jiji la Dar es Salaam alijitokeza kuwa mshindi kwenye mashindano hayo, na baadaye mwaka huu atashiriki katika mashindano ya kwanza ya “Daraja la Lugha ya Kichina” kwa ajili ya wanafunzi wa shule za msingi za nchi mbalimbali duniani yatakayofanyika nchini China.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Renato Lu)

Picha