Vikosi vya Uganda na DRC vyakamata silaha kutoka waasi wa kundi la ADF

(CRI Online) Mei 11, 2024

Msemaji wa tawi la mlima la Jeshi la Uganda (UPDF) Bilal Katamba Alhamisi alisema vikosi vya Uganda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) vilipata silaha za waasi wa kundi la ADF huko misitu iliyoko mashariki mwa DRC.

Katamba alisema silaha hizo ziligunduliwa kwenye opresheni za kijeshi za pamoja dhidi ya kundi la ADF. Silaha hizo zilizofichwa ziligunduliwa Jumatano kwenye Eneo la Tatu lililoko karibu na Daraja la Mto Talia mkoani Kivu Kaskazini nchini DRC.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Renato Lu)

Picha