

Lugha Nyingine
Israel yaamuru tena kuhamishwa kwa watu huko Rafah baada ya kura za UN kuunga mkono uanachama wa Palestina
Israel imetoa amri nyingine siku ya Jumamosi ya kuhamishwa watu katika mji wa kusini mwa Gaza wa Rafah wakati ikijiandaa kuzidisha operesheni yake ya kijeshi, ikiwa ni siku moja baada ya Umoja wa Mataifa (UN) kupitisha azimio la kuidhinisha ombi la Wapalestina la kutaka uanachama kamili wa Umoja wa Mataifa.
Azimio hilo lililopitishwa kwa kura 143 za ndiyo na tisa zikipiga kura ya hapana, zikiwemo Marekani na Israel, huku nchi 25 zikijizuia, limeonesha uungaji mkono unaoongezeka kwa Wapalestina, huku nchi nyingi zikielezea kukerwa na kuongezeka kwa idadi ya vifo huko Gaza na kuwa na wasiwasi juu ya uwezekano mkubwa wa mashambulizi ya Israeli huko Rafah.
Wapalestina zaidi ya milioni 1 waliokimbia makazi yao wanatafuta hifadhi Rafah, ambako janga kubwa la kibinadamu linakaribia kutokana na uhaba wa vitu muhimu kama vile maji, chakula na huduma za matibabu. Sasa, mji huo uko ukingoni kuwa na mgogoro mpya.
Umoja wa Mataifa umeonya kuwa uvamizi wa Rafah utazidisha janga la kibinadamu na kusababisha kuongezeka kwa vifo vya raia.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma