Mfuko wa CFRD wa China wasifiwa kwa kuimarisha huduma za kibinadamu nchini Ethiopia

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Mei 13, 2024

Hafla ya uzinduzi wa Mradi wa Kujitolea wa Kampuni za China nchini Ethiopia ikifanyika Addis Ababa, Ethiopia, Mei 10, 2024. (Xinhua/Michael Tewelde)

Hafla ya uzinduzi wa Mradi wa Kujitolea wa Kampuni za China nchini Ethiopia ikifanyika Addis Ababa, Ethiopia, Mei 10, 2024. (Xinhua/Michael Tewelde)

ADDIS ABABA – Mfuko wa China Kwa Maendeleo Vijijini (CFRD) umesifiwa kwa kuimarisha msaada wa kibinadamu nchini Ethiopia wakati ukiadhimisha miaka yake mitano tangu uanze kufanya kazi katika nchi hiyo ya Afrika Mashariki kwenye hafla maalum iliyofanyika siku ya Ijumaa huko Addis Ababa, mji mkuu wa Ethiopia ambayo pia ilishuhudia kuanzishwa kwa Mradi wa Kujitolea wa Kampuni za China nchini humo.

Akizungumza kwenye hafla hiyo iliyoshirikishwa na maofisa waandamizi wa serikali ya Ethiopia, wanadiplomasia wa China na wawakilishi wa kampuni za China, Waziri wa Wanawake na Mambo ya Kijamii wa Ethiopia, Ergogie Tesfaye amesema pamoja na miradi yake ya kutoa chakula kwa wanafunzi, maji na usafi wa mazingira mashuleni, kupunguza umaskini na kuwezesha wanawake kiuchumi, CFRD imetoa msaada kwa watu 320,000 nchini Ethiopia.

"Leo nimejawa na furaha kushuhudia mafanikio ya Mfuko wa China kwa Maendeleo Vijijini nchini Ethiopia ambao mchango wake wa kuleta mabadiliko makubwa katika maisha ya watu nchini Ethiopia unastahili kupongezwa," Tesfaye amesema.

Kwa "Mradi wa kuwafanya Watoto Watabasamu", CFRD imekuwa ikishirikiana na serikali ya Ethiopia na mashirika yasiyo ya kiserikali (NGOs) ya nchini humo ili kufikia lengo la mradi wake wa "kutokuwepo kwa njaa" nchini Ethiopia, hasa kupitia miradi ya kutoa chakula wanafunzi mashuleni na kupunguza umaskini.

Akisisitiza kwamba CFRD imefanya kazi nyingi katika kuimarisha uhusiano kati ya watu wa China na Ethiopia, Yang Yihang, balozi mdogo wa China nchini Ethiopia, amesema CFRD imekuwa ikishughulikia mahitaji mbalimbali ya jamii maskini nchini Ethiopia katika kipindi cha miaka mitano iliyopita.

"CFRD imekuwa ikifanya miradi mingi ya ufadhili nchini Ethiopia kupitia mpango wa kutoa chakula kwa wanafunzi mashuleni, mradi wa kuzawadia mkoba wa shule wa panda na mradi wa taa zinazotumia nishati ya jua miongoni mwa mingine," Yang amesema.

Kwa mujibu wa habari zilizopatikana katika hafla hiyo, CFRD imewekeza dola zaidi ya milioni 10.5 za Kimarekani kutekeleza huduma zake za kibinadamu nchini Ethiopia.

Waziri wa Wanawake na Mambo ya Kijamii wa Ethiopia Ergogie Tesfaye akizungumza katika hafla mjini Addis Ababa, Ethiopia, Mei 10, 2024. (Xinhua/Michael Tewelde)

Waziri wa Wanawake na Mambo ya Kijamii wa Ethiopia Ergogie Tesfaye akizungumza katika hafla mjini Addis Ababa, Ethiopia, Mei 10, 2024. (Xinhua/Michael Tewelde)

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha