Rwanda yapinga tuhuma za Burundi kuhusu kuhusika na mashambulizi ya makombora

(CRI Online) Mei 13, 2024

Serikali ya Rwanda imepinga tuhuma za Burundi kuhusu kuhusika kwake na mashambulizi ya makombora yaliyotokea katika stendi ya basi iliyoko katika mji mkuu wa Burundi, Bujumbura, Ijumaa ya wiki iliyopita, ambapo watu 40 walijeruhiwa.

Baada ya tukio hilo, Polisi nchini Burundi na Wizara ya Mambo ya Ndani ya nchi hiyo waliituhumu serikali ya Rwanda kwa kuhusika na mashambulizi hayo, wakidai imeshirikiana na kundi la waasi la Red Tabara ambalo Burundi inadai linaungwa mkono na serikali ya Rwanda.

Katika taarifa iliyotolewa jana Jumapili, Ofisi ya Msemaji wa Serikali ya Rwanda imepinga vikali madai hayo, na kuitaka Burundi kutatua matatizo yake ya ndani yenyewe bila ya kuihusisha Rwanda.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha