Misri "kuunga mkono rasmi" kesi ya mauaji ya halaiki iliyowasilishwa na Afrika Kusini dhidi ya Israel katika mahakama ya ICJ

(CRI Online) Mei 13, 2024

Misri imetangaza jana Jumapili kwamba "itaunga mkono rasmi" kesi ya mauaji ya halaiki iliyofunguliwa na Afrika Kusini dhidi ya Israel katika Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ) kuhusu uvamizi unaoendelea wa Israel katika Ukanda wa Gaza huko Palestina.

Tangazo hilo lililotolewa na Wizara ya Mambo ya Nje ya Misri, limekuja kutokana na "kuendelea kwa Israel kufanya mashambulizi dhidi ya watu wa Palestina, ikiwa ni pamoja na kuwalenga raia, kufanya uharibifu wa miundombinu katika eneo hilo, na kulazimisha Wapalestina kuhama kwenye ardhi yao."

Mashambulizi ya Israel "yamesababisha janga la kibinadamu ambalo halijawahi kushuhudiwa na kusababisha watu wasiweze kuishi katika Ukanda wa Gaza, kutokana na ukiukaji wa wazi wa vifungu vya sheria za kimataifa na sheria za kimataifa za kibinadamu.

Hata hivyo taarifa hiyo haikufafanua ni aina gani ya uungwaji mkono utakaotolewa kwa Afrika Kusini katika kesi hiyo. Tangazo hilo limekuja baada ya Afrika Kusini siku ya Ijumaa kuitaka mahakama ya ICJ kutoa amri mpya kwa Israel kusitisha mara moja operesheni yake katika eneo la Rafah na kujiondoa katika mji huo wa kusini mwa Gaza.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha