Umoja wa Mataifa wasema watu milioni 7.1 watakumbwa na matatizo ya usalama wa chakula nchini Sudan Kusini hadi Julai

(CRI Online) Mei 14, 2024

Shirika la Kuratibu Misaada ya Kibinadamu la Umoja wa Mataifa (OCHA) limesema watu wasiopungua milioni 7.1 wanaweza kukumbwa na ukosefu mkubwa wa chakula nchini Sudan Kusini kati ya Aprili na Julai.

Ripoti mpya iliyotolewa Jumapili jioni na OCHA imesema hadi tarehe 30 Aprili, mgogoro wa Sudan umesababisha watu 655,694 wakimbie makazi yao nchini humo na kwenda Sudan Kusini, ambapo kwa wastani watu takriban 1,800 wanaingia Sudan Kusini kila siku.

Kwa mujibu wa OCHA, watu elfu 79 wako katika hali ya maafa, ambapo wengi wao wanaishi katika maeneo yanayokabiliwa na athari ya tabianchi, kuyumba kwa uchumi, au mapigano.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha