

Lugha Nyingine
Rais Putin wa Russia kufanya ziara ya kiserikali nchini China Mei 16 hadi 17
BEIJING – Kutokana na mwaliko wa Rais wa China Xi Jinping, Rais wa Russia Vladimir Putin atafanya ziara ya kiserikali nchini China kuanzia Mei 16 hadi 17, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China, Hua Chunying ametangaza jana siku ya Jumanne.
Hii ni ziara ya kwanza ya Putin baada ya kuapishwa kuwa Rais wa Russia kwa awamu mpya, Wang Wenbin, msemaji mwingine wa wizara hiyo ameuambia mkutano na waandishi wa habari baadaye siku hiyo.
Huku mwaka huu ukiwa ni maadhimisho ya miaka 75 tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia kati ya China na Russia, katika ziara hiyo Putin, rais Xi na Putin watabadilishana mawazo kuhusu uhusiano wa pande mbili, ushirikiano katika sekta mbalimbali, na masuala ya kimataifa na ya kikanda yanayofuatiliwa kwa pamoja na pande hizo mbili.
Ameongeza kuwa China itatoa taarifa muhimu kuhusu ziara hii kwa wakati ufaao.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma