Ethiopia yapongeza uwekezaji wa China katika sekta ya nguo

(CRI Online) Mei 15, 2024

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Maendeleo ya Maeneo Maalumu ya Viwanda nchini Ethiopia Aklilu Tadesse amesema, uwekezaji wa China ni injini muhimu katika sekta ya nguo na vitambaa nchini Ethiopia, na kwamba wawekezaji wa China ni msingi muhimu wa maendeleo ya sekta hiyo nchini Ethiopia.

Tadesse ameyasema hayo jana siku ya Jumanne wakati wa majadiliano kati ya maofisa kutoka Shirikisho hilo na Kamisheni ya Uwekezaji ya Ethiopia pamoja na kampuni za China zinazotaka kuwekeza katika sekta ya nguo na vitambaa nchini Ethiopia.

Akizungumzia mchango mkubwa wa sekta hiyo katika uchumi wa Ethiopia, Tadesse amesema uwekezaji katika sekta hiyo ni kichocheo kikubwa cha maendeleo na ukuaji wa jumla wa uchumi wa Ethiopia, huku akiongeza kuwa, sekta hiyo imetoa ajira za kudumu na za muda mfupi kwa maelfu ya Waethiopia.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha