China yasema Reli ya Addis Ababa-Djibouti inachochea maendeleo ya uchumi wa Ethiopia na Djibouti

(CRI Online) Mei 15, 2024

Mkutano wa kutangaza matokeo ya miaka sita iliyopita na mtazamo wa siku za usoni kuhusu Reli ya Addis Ababa-Djibouti ambao pia ni hafla ya kukabidhi ufunguo umefanyika hivi karibuni mjini Addis Ababa nchini Ethiopia.

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Bw. Wang Wenbin amesema siku ya Jumanne kuwa reli hiyo ni mradi wa kujenga kwa pamoja pendekezo la “Ukanda Mmoja, Njia Moja” kati ya China na Ethiopia na Djibouti, ambao umewapatia watu wenyeji zaidi ya elfu 55 nafasi za ajira tangu ilipomalizika kujengwa, pia inachochea zaidi maendeleo ya uchumi wa Ethiopia na Djibouti.

Ameongeza kuwa hafla hiyo inamaanisha kuwa huduma ya uendeshaji na ukarabati kwa reli hiyo kwa upande wa China imemalizika, na sasa upande wa nchi hizo mbili unaendesha reli hiyo kikamilifu.

Amesema, China itaendelea kushirikiana na Ethiopia na Djibouti, na kuifanya reli hiyo kuwa njia yenye ustawi katika kuhimiza ushirikiano wa kunufaishana.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha