

Lugha Nyingine
Warizi Mkuu wa Slovakia aripotiwa kuwa katika hali ya mahututi baada ya kupigwa risasi
(CRI Online) Mei 16, 2024
Waziri Mkuu wa Slovakia Robert Fico ameripotiwa kuwa katika hali mahututi baada ya kupigwa risasi mjini Handlova, eneo la Trencin nchini Slovakia.
Mshukiwa aliyezuiliwa papo hapo anaripotiwa kuwa mzee wa miaka 71.
Shirika la Habari la Slovakia TASR limemnukuu makamu mwenyekiti wa bunge la Slovakia Lubos Blaha akisema kuwa tukio hilo limetokea wakati wa kikao cha bunge. Bunge hilo limeahirishwa hadi itakapotangazwa tena.
Kwa mujibu wa kituo cha televisheni cha TA3, tukio hilo limetokea katika mji wa Handlova, takriban umbali wa kilomita 150 kaskazini mashariki mwa mji mkuu. Polisi wamefunga eneo hilo mbele ya Jumba la Utamaduni huko Handlova.
(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma