

Lugha Nyingine
Rais wa Uganda awasili Kenya kwa ziara ya siku tatu
(CRI Online) Mei 16, 2024
Rais Yoweri Museveni wa Uganda amewasili Nairobi, Kenya kwa ziara ya kiserikali ya siku tatu, ambako anatarajiwa kukutana na kufanya mazungumzo na mwenzake wa Kenya Williams Ruto siku ya Alhamisi.
Ziara hiyo inafuatia kikao cha pili cha Tume ya Pamoja ya Mawaziri (JMC) kilichomalizika hivi karibuni kati ya Kenya na Uganda, ambapo makubaliano saba ya maelewano yalisainiwa katika maeneo ya usimamizi wa huduma za umma, elimu, maendeleo ya kampuni ndogo na zenye ukubwa wa kati, michezo, vijana, biashara, na uwekezaji.
(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma