Vyombo vya habari vya Afrika vyahimizwa kukumbatia teknolojia ya kidijitali ili kubadilisha fikra potofu kuhusu Afrika

(CRI Online) Mei 17, 2024

Mkurugenzi wa habari na mawasiliano wa Umoja wa Afrika Leslie Richer amesema vyombo vya habari vya Afrika vinapaswa kutumia nguvu ya teknolojia ya kidijitali kueleza simulizi ya Afrika, na kubadilisha simulizi na mitazamo kuhusu bara hilo duniani kote.

Akitoa wito huo kwenye hotuba yake ya ufunguzi wa Mkutano wa 3 wa Vyombo vya Habari vya Afrika (AMC), ulioanza mjini Accra, nchini Ghana siku ya Jumatano, Bi. Richer amesema kwa kutumia zana za uchambuzi wa data, vyombo vya habari vya Afrika vinaweza kuthibitisha chanzo na uhalisi wa data zinazotumika kuelezea na kutathmini bara na watu wake duniani, na kusahihisha simulizi zisizo sahihi.

“Huku kukiwa na teknolojia inayoendelea kubadilika na mazingira ya vyombo vya habari vya kidijitali, simulizi kuhusu Afrika na Waafrika ni muhimu zaidi. Ni lazima tuhoji chanzo cha data ambazo zinatumika kufafanua na kutuelezea sisi duniani,” Richer amesema.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha