Serikali ya Sudan Kusini na makundi ya upinzani wasaini makubaliano ya kufikia amani ya kudumu

(CRI Online) Mei 17, 2024

Serikali ya Mpito ya Umoja wa Kitaifa ya Sudan Kusini na makundi ya upinzani wamesaini makubaliano kwa ajili ya kuimarisha juhudi za kufikia amani na utulivu wa kudumu nchini humo siku ya Alhamisi.

Kwa kusaini azimio la mpango wa Tumaini, pande hizo mbili zimeahidi kuunga mkono jitihada za kusimamisha uhasama na kuhimiza ukuaji jumuishi nchini Sudan Kusini.

Hafla ya kusaini makubaliano hayo iliyofanyika mjini Nairobi nchini Kenya, ilihusisha maofisa wa ngazi ya juu wa serikali, wanadiplomasia, makundi ya upinzani, asasi za kijamii na washirika wa pande mbili.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Diaspora ya Kenya Abraham Korir SingOei, amepongeza kusainiwa kwa makubaliano hayo, ambayo yatahimiza kufikiwa kwa amani, haki, ujumuishaji na utawala bora nchini Sudan Kusini.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha