Lugha Nyingine
Kenya yarejesha huduma za intaneti baada ya nyaya za chini ya bahari kukatika
Mamlaka ya Mawasiliano ya Kenya (CA) na kampuni kubwa ya simu za mkononi ya Safaricom nchini humo, zimethibitisha kurejea kwa huduma za intaneti siku ya Alhamisi ikiwa ni siku nne baada ya kukosekana kutokana na kukatika mara kwa mara kwa nyaya za chini ya bahari.
Mamlaka hizo zimetangaza kuwa huduma ya mtandao imerejeshwa kwa uwezo wake kamili na ni thabiti baada ya watumiaji kupata kasi ndogo iliyosababishwa na kukatika kwa nyaya chini ya bahari katika kituo cha mawasiliano cha Mtunzini nchini Afrika Kusini siku ya Jumapili.
Hata hivyo, Mamlaka ya Mawasiliano nchini Kenya imeonya kuwa kuondoa tatizo hilo lililosababishwa na kukatika kwa nyaya kunaweza kuchukua muda.
Ukatikaji huo uliathiri nyaya nyingi zinazohudumia Kenya, zikiwemo za Mfumo wa Nyaya za Chini ya Bahari wa Afrika Mashariki (EASSy) na nyaya za Seacom.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



