Magofu ya Yin: Sikia mwangwi wa miaka 3,000 iliyopita

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Mei 18, 2024

“Kwa muda mrefu nimekuwa nikitamani kutembelea magofu ya Yin. Mara hii nimekuja hapa kujifunza zaidi kuhusu ustaarabu wa China, na kutumia mambo ya kale katika ya sasa, na kutoa rejeleo kwa ajili ya kujenga vizuri zaidi ustaarabu wa taifa la China wa zama za sasa,” alisema Rais Xi Jinping alipofanya ziara ya ukaguzi kwenye magofu ya Yin katika Mji wa Anyang, Mkoa wa Henan wa China mwezi Oktoba, 2022.

Magofu hayo ya Yin yenye historia ya zaidi ya miaka 3,000 yamethibitisha kabisa kuwepo kwa hadithi ya enzi ya Yin.

Tarehe 26, Februari, 2024, Jumba la Makumbusho la Enzi ya Yin lilifunguliwa rasmi, huku seti za mabaki ya kitamaduni 4,000, vikiwemo vyombo vya shaba nyeusi yakioneshwa kwa umma.

Hivi karibuni, waandishi wa habari wa People’s Daily Online walitembelea jumba hilo la makumbusho.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha