Anyang,Henan:Mji wa Kale wa Enzi ya Shang wapata nguvu zaidi ya maendeleo ya kiuchumi

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Mei 18, 2024

Anyang ni mji maarufu wa kihistoria na kiutamaduni wa China, na ni moja ya miji minane wa kale nchini China. Mji huo una mali nyingi za urithi wa utamaduni, na utamaduni wake unahusisha mambo mengi mbalimbali. Kwa kupitia maelfu ya miaka, mji huo umekuwa na mvuto wake wa kipekee katika vipindi tofauti. Utamaduni wa Enzi ya Shang wa zaidi ya miaka 3000 iliyopita unaendelea kizazi baada ya kizazi, moyo wa Mfereji wa Bendera Nyekundu uliojengwa kwa kujitegemea unaenziwa bila kusita. Anyang inajulikana ni “mji wenye nguvu ya kuruka”, ambao michezo ya usafiri wa anga ilianzishwa mapema mjini humo, na shughuli za huduma za usafiri wa anga unaohusika na sekta mbalimbali pamoja na shughuli za roboti zimeendelea vizuri, uchumi huo wa eneo la mbingu wa chini umekuwa kichocheo cha ongezeko jipya katika shughuli za biashara na nyingine mbalimbali za kuimarisha nguvu ya mji wa Anyang.

Siku za hivi karibuni, waandishi wa habari wa People’s Daily Online wametembelea huko Anyang wakijihisi mvuto wa mji huo wa kale wenye uhai.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha