Waziri wa Mambo ya Nje wa China afanya mazungumzo na mwenzake wa Tanzania

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Mei 20, 2024

Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi, akifanya mazungumzo na January Yusuf Makamba, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wa Tanzania mjini Beijing, China, Mei 17, 2024. (Xinhua/Liu Bin)

BEIJING - Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi amefanya mazungumzo na January Yusuf Makamba, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wa Tanzania mjini Beijing siku ya Ijumaa iliyopita ambapo amekaribisha ziara hiyo ya Makamba nchini China wakati wa maadhimisho ya miaka 60 tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia kati ya nchi hizo mbili.

Wang, ambaye pia ni mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China amesema uhusiano kati ya China na Tanzania siku zote umekuwa mstari wa mbele katika uhusiano kati ya China na Afrika katika miaka 60 iliyopita, jambo ambalo ni mfano mzuri kwa nchi zinazoendelea kutafuta nguvu kupitia mshikamano na kusaidiana.

Wang amesema, China ingependa kuongeza hali ya kuaminiana kisiasa, kuimarisha kuendana kimkakati, kupanua ushirikiano wa matokeo halisi na kuingiza maana mpya ya zama katika uhusiano wa wenzi wa ushirikiano wa kimkakati wa pande zote kati ya China na Tanzania chini ya makubaliano muhimu yaliyofikiwa na wakuu wa nchi hizo mbili.

Amesema China inathamini uungaji mkono wa thamani wa muda mrefu wa Tanzania katika masuala yanayohusu maslahi makuu ya China, na ingependa kuendelea kuiunga mkono Tanzania kwa uthabiti katika kulinda mamlaka ya nchi, usalama na maslahi yake ya maendeleo, na kutafuta kwa kujiamulia yenyewe njia ya maendeleo inayoendana na hali halisi ya nchi yake .

Pande hizo mbili zinapaswa kupanua ushirikiano katika maeneo muhimu kama vile biashara na miundombinu, na uwezekano wa ushirikiano katika utengenezaji na uzalishaji bidhaa, uchumi wa kidijitali, uchumi wa bluu na nishati mpya, Wang ameongeza.

Na waziri Makamba amesema, Tanzania na China zina urafiki mkubwa wa jadi, nchi hizo mbili zimekuwa zikiaminiana na kusaidiana tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia miaka 60 iliyopita.

Kufuata sera ya kuwepo kwa China moja ndiyo msingi wa uhusiano wa Tanzania na China, na Tanzania itaendelea kuiunga mkono China bila kuyumbayumba katika masuala yanayohusu maslahi ya msingi na mambo makuu yanayofuatiliwa na China.

Amesema, Tanzania inatarajia kuboresha mabadilishano ya uzoefu kuhusu usimamizi wa mambo, kuimarisha ushirikiano wa kunufaishana katika sekta mbalimbali na kushirikiana kwa karibu na China katika masuala ya kimataifa na kikanda.

Amesema, Tanzania itashiriki kikamilifu katika mkutano wa Baraza la Ushirikiano wa China na Afrika mwaka huu na inaamini kuwa mkutano huo utapata mafanikio makubwa zaidi.

Pande hizo mbili pia zimebadilishana maoni ya kina kuhusu masuala ya kimataifa na ya kikanda yanayofuatiliwa nazo kwa pamoja.

Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi, akifanya mazungumzo na January Yusuf Makamba, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wa Tanzania mjini Beijing, China, Mei 17, 2024. (Xinhua/Liu Bin)

Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi, akifanya mazungumzo na January Yusuf Makamba, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wa Tanzania mjini Beijing, China, Mei 17, 2024. (Xinhua/Liu Bin)

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha