

Lugha Nyingine
Mashindano mfululizo ya kwanza ya Marathon ya Wafanyakazi wa China zilianza Mji wa Rizhao
Mashindano mfululizo ya Marathon ya Wafanyakazi wa China 2024, yenye kaulimbiu ya “Ndoto ya China Uzuri wa Kazi—Kukimbia kwa Maisha Bora” zilianza katika hali motomoto katika Mji wa Rizhao, washiriki kutoka sehemu na sekta mbalimbali nchini kote walikusanyika katika Mji wa Rizhao, Mkoa wa Shandong.
Mashindano hayo ya Marathon yamewekwa mashindano matatu, mbio nusu za Marathon(kilomita 21.0975), mbio za kikosi cha kuongoza (kilomita 6.6) na mbio za afya (kilomita 2.5).
Miongoni mwao, kundi la wafanyakazi wa mifano ya kuigwa la mbio za kikosi cha kuongoza linaundwa na wafanyakazi na watu wa mifano ya kuigwa 6,000, wakiwemo mfanyakazi wa mfano wa kuigwa Jia Tingbo, mfanyakazi bora wa kitaifa Zhang Nianhua, mshindi wa nishani ya kitaifa ya Mei Mosi , Zhang Nianli, na mfanyakazi bora wa Mkoa wa Shandong Zhang Lanxiang, washindi wa nishani ya Mei Mosi ya Mkoa wa Shandong, Qin Yuhua na Meng Lingxin, pamoja na wafanyakazi wa mfano wa kuigwa wa Mji wa Rizhao na wafanyikazi wengine, walionyesha vilivyo hali sura nzuri na nguvu kubwa za wafanyakazi kutoka sekta mbalimbali.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma