Kutoa heshima kwa "uzuri wa kazi" kupitia kukimbia

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Mei 20, 2024

Mashindano ya mfululizo ya kwanza ya Marathon ya Wafanyakazi wa China 2024 (Kituo cha Nusu Marathon cha Rizhao) ikianza rasmi kwa kufyatuliwa mlio wa kuashiria kuanza.

Mashindano ya mfululizo ya kwanza ya Marathon ya Wafanyakazi wa China 2024 (Kituo cha Nusu Marathon cha Rizhao) ikianza rasmi kwa kufyatuliwa mlio wa kuashiria kuanza.

Shirikisho Kuu la Wafanyakazi wa nchi nzima ya China limeanzisha mashindano mfululizo ya kwanza ya marathon ya wafanyakazi kuanzia Mei hadi Desemba mwaka huu ili kufanya shughuli ya mbio barabarani mahususi kwa wafanyakazi ambayo ni tofauti na mbio nyingine za marathon mijini.

Kaulimbiu ya mbio hizo ni "Ndoto ya China Uzuri wa Kazi—Kukimbia kwa Maisha Bora", ikiangazia umaalum wa mashirikisho ya wafanyakazi na wafanyakazi. Mashidano hayo ya marathon yamepangwa kufanywa kwenye vituo vitatu kila mwaka, ambapo wakimbiaji jumla watafikia 60,000 hivi, na Mji wa Rizhao katika Mkoa wa Shandong ndiyo kituo cha kwanza katika mfululizo wa mbio hizo.

Asubuhi ya Mei 19, mashindano mfululizo ya marathoni ya wafanyakazi (Kituo cha Nusu Marathon cha Rizhao), yanayoelekezwa na Shirikisho kuu la wafanyakazi, na kuandaliwa na Shirika la Utalii wa Kimataifa la Wafanyakazi wa China na Serikali ya Umma ya Rizhao, yalianza rasmi. Wafanyakazi kutoka sehemu mbalimbali nchini na wa sekta mbalimbali walifika kwenye sehemu ya kuanzia mbio hizo. Wanariadha wafanyakazi wapatao 15,000 kutoka sekta mbalimbali walikusanyika kwenye "njia nzuri zaidi" ya kukimbilia huko Rizhao.

Mashindano hayo ya marathon yanahusisha mbio za nusu marathon, mbio za kikosi cha kuongoza na mbio za afya, ambayo yataonyesha mtindo na maisha ya kiafya ya wafanyakazi wa China katika michezo, na kuongoza wafanyakazi wengi kuchukua hatua kwa hamasa kubwa zaidi ya kazi na moyo thabiti. Kujitoa kwenye kazi na maisha kwa afya njema.

Katika nafasi zao za kazi, wafanayakazi wamejaa hamasa na kukabiliana na kila changamoto; kwenye uwanja wa michezo, wamejaa vilevile nguvu. Kwenye eneo la mashindano, timu ongozi ya mbio za mraba inayojumuisha wafanyakazi na watu wa mfano wa kuigwa kutoka sekta mbalimbali ilivutia sana.

Wafanyakazi wa mfano wa kuigwa wa kitaifa Jia Tingbo, Wang Juni na Qu Wanchong, washindi wa kitaifa wa Medali ya Kazi ya Mei Mosi, Zhang Nianli na Li Yajun, mfanyakazi bora wa kitaifa Zhang Nianhua, fundi mstadi wa kitaifa Peng Chengmin na wajumbe wengine wa wafanyakazi waliosifiwa walionekana uwanjani na kukimbia kwa kuchangamana na kila mtu.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha