China yarahisisha mchakato wa usafiri wa kimataifa ili kukidhi mahitaji ya watalii wanaosafiri nchi za nje

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Mei 20, 2024

BEIJING - Mapema mwezi Aprili, Xiao Ying na mumewe walianza safari ya ndege kutoka Beijing hadi Geneva, wakianza mapumziko yao ya fungate katika miji ya kupendeza ya Uswizi.

Ndege hiyo, ambayo ilikuwa imesimamishwa wakati wa janga la UVIKO-19, ilianza tena kazi mwezi Februari 2023, ikiashiria ufufukaji muhimu katika utalii kwa wasafiri wa China.

"Ndege hiyo iliyoanza tena kutoa huduma imetupa machaguo ya kusafiri," Xiao amesema.

Katika robo ya kwanza ya Mwaka 2024, watalii wa China Bara walikaa jumla ya usiku 153,723 nchini Uswizi, ikiwa ni ongezeko la asilimia 92.2 kutoka kipindi kama hicho mwaka jana, kwa mujibu wa takwimu kutoka idara ya Utalii wa Uswizi.

"Kurejeshwa kwa safari za ndege kati ya nchi hizi mbili kunachangia kwa kiasi kikubwa ongezeko la watalii wa China," amesema Shi Bang, mkurugenzi wa bodi ya Kampuni Wakala wa Utalii ya LOTO AG yenye makao yakel Uswizi. "Pia, taratibu za visa zimerahisishwa kwa wasafiri wa China."

Ili kukidhi mahitaji yanayoongezeka ya safari za nje, China imeongeza uwezo wa ndege na kupanua sera nzuri za visa kwa raia wake.

Kwa mujibu wa Idara ya Usafiri wa Anga ya China (CAAC), safari za ndege za abiria za kimataifa zimerejea kwa takriban asilimia 73 ya viwango vyake vya kabla ya janga.

Mwezi Aprili, idadi ya safari za ndege kati ya China na nchi kama vile Uingereza, Falme za Kiarabu (UAE), Italia, Qatar na Uturuki ilizidi zile za kipindi kama hicho Mwaka 2019, kwa mujibu wa ripoti ya Flight Manager, shirika shirika ambalo linatoa huduma za habari za anga.

Kwa sasa, safari za ndege za kimataifa za abiria zinaunganisha China na nchi 70, huku maeneo matano mapya yakiwa yameongezwa tangu janga la COVID: Kuwait, Serbia, Tanzania, Luxembourg, na Papua New Guinea. Hivi karibuni, njia mpya za kimataifa zimeanzishwa, zikijumuisha njia ya Beijing-Madrid-Sao Paulo na njia ya Mji wa Shenzhen-Mexico, CAAC imesema.

Zaidi ya hayo, China inatekeleza sera ya kuondoa hitaji la visa kwa nchi kadhaa ili kurahisisha usafiri kwa raia wa nchi hizo.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha