

Lugha Nyingine
"Jaribio la mapinduzi" mjini Kinshasa lazimwa na "hali iko katika udhibiti" - Jeshi la DRC
Picha hii iliyopigwa kwa simu ya mkononi tarehe 19 Mei, 2024 ikionyesha mandhari ya Kinshasa, mji mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC). (Str/Xinhua)
KINSHASA - "Jaribio la mapinduzi" huko Kinshasa, mji mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), limezimwa siku ya Jumapili na vikosi vya ulinzi na usalama, amesema Sylvain Ekenge, msemaji wa Jeshi la DRC. "Jeshi linawahakikishia kuwa hali imedhibitiwa na linawaambia wakaazi wa Kinshasa kufanya shughuli zao kwa uhuru," amesema.
Msemaji huyo amesema katika ujumbe mfupi uliotangazwa kwenye televisheni ya umma, akibainisha kuwa wahusika kadhaa wa tukio hilo wamekamatwa.
Vifo takriban watu watatu vimeripotiwa katika mapambano mapema Jumapili na kundi la washambuliaji katika vitongoji ambako wanasiasa na wajumbe wa kidiplomasia wanakoishi mjini Kinshasa, kwa mujibu wa vyombo vya habari vya DRC.
Kwa mujibu wa mashuhuda, "milio mizito ya risasi" ilisikika majira ya saa 10:30 jioni (0330 GMT) siku ya Jumapili karibu na makazi ya Vital Kamerhe, mbunge wa kitaifa na mgombea wa spika wa Bunge la Taifa, ambalo ni baraza la chini la bunge hilo.
Watu watatu, ikiwa ni pamoja na maafisa wawili wa polisi, wameuawa katika mapigano hayo, vyombo vya habari vya DRC vimeripoti, vikinukuu vyanzo vya usalama.
Washambuliaji hao pia waliingia Palais de la Nation, makao makuu ya heshima ya urais wa DRC huko Kinshasa, na kusema kupitia matangazo ya moja kwa moja kwenye Facebook kwamba "wanapigania nchi."
Rais wa DRC Felix Tshisekedi anafanya kazi hasa katika Cite de l'Union Africaine (Mji wa Umoja wa Afrika), jengo la serikali katika wilaya ya Ngaliema ya Kinshasa. Msemaji wa jeshi hakutoa maelezo kuhusu hali ya rais au Kamerhe.
Michel Moto Muhima, msemaji wa Kamerhe, amesema kwenye mtandao wa kijamii wa X kwamba Kamerhe na familia yake walikuwa "salama na wazima" na kwamba "ulinzi wao umeimarishwa."
Picha hii iliyopigwa kwa simu ya mkononi tarehe 19 Mei, 2024 ikionyesha mandhari ya Kinshasa, mji mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC). (Str/Xinhua)
Picha hii iliyopigwa kwa simu ya mkononi tarehe 19 Mei, 2024 ikionyesha mandhari ya Kinshasa, mji mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC). (Str/Xinhua)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma