

Lugha Nyingine
China yaitaka Marekani kuacha kutoa ishara zisizo sahihi kwa vikundi vya kutaka "Taiwan Ijitenge"
BEIJING - Chen Binhua, Msemaji wa Ofisi ya Mambo ya Taiwan ya Baraza la Serikali la China siku ya Jumatatu ameitaka Marekani kuacha kutoa ishara zisizo sahihi kwa vikundi vinavyofanya shughuli za kutaka "Taiwan Ijitenge" .
Chen ameyasema hayo wakati akijibu swali la vyombo vya habari kuhusu Marekani na hatua ya baadhi ya nchi kutuma watu kushiriki kwenye hafla ya Lai Ching-te kushika madaraka ya kuwa kiongozi mpya wa Taiwan.
"Tunapinga vikali aina yoyote ya mawasiliano ya kiserikali kati ya eneo la Taiwan ya China na Marekani na nchi nyingine zenye uhusiano wa kidiplomasia na China. Tunalaani vikali kuingilia kati mambo ya Taiwan kwa kisingizio chochote au kwa mbinu yoyote," Chen amesema.
"Tunautaka upande wa Marekani na nchi husika kurekebisha mara moja makosa yao na kuacha kutoa ishara zisizo sahihi kwa vikundi vinavyotaka 'Taiwan Ijitenge'," ameongeza.
Jaribio la watawala wa Chama cha Kidemokrasia cha Taiwan kutafuta uungaji mkono na uingiliaji kutoka nje kwa ajili ya Taiwan kujitenga hakutazuia mwelekeo usioweza kurudishwa nyuma wa muungano wa Taifa la China, Chen amesema.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma