

Lugha Nyingine
Mtandao wa rada uliojengwa na China kuunga mkono utabiri wa hali ya hewa ya anga ya juu duniani
Picha hii ya kumbukumbu isiyo na tarehe iliyotolewa na Kituo cha Taifa cha Sayansi ya Anga ya Juu cha China (NSSC) ikionyesha rada zilizoko Mkoa unaojiendesha wa Kabila la Wauygur wa Xinjiang, Kaskazini-Magharibi mwa China. (Xinhua)
BEIJING - China imejenga mtandao wa rada ulioko latitude ya kati katika maeneo ya kaskazini mwa nchi hiyo ili kutoa huduma ya unasaji wa data wa hali ya juu kwa ajili ya utabiri na tahadhari za hali ya hewa ya anga ya juu duniani.
Matokeo ya kwanza ya unasaji wa kisayansi wa mtandao huo yametolewa kwenye semina ya kimataifa ya Mtandao wa Rada wa Super Dual Auroral (SuperDARN), ambayo imefunguliwa Beijing siku ya Jumatatu.
Mtandao huo, uliojengwa na Kituo cha Taifa cha Sayansi ya Anga ya Juu cha China (NSSC) chini ya Akademia ya Sayansi ya China, ulikamilika Oktoba 2023. Pia ni sehemu ya awamu ya pili ya Mradi wa Meridian wa China, ambao ni mtandao wa kufuatilia hali ya hewa ya anga ya juu unaojumuisha vituo vilivyoko ardhini.
China imepata maendeleo mapya katika teknolojia ya rada na utafiti wa kisayansi, na itaimarisha ushirikiano wa kimataifa katika nyanja hii, imesema NSSC.
Ionosphere ni nyumbani mwa chembe zote zilizochajiwa katika angahewa la dunia. Pia ni nyumbani mwa vyombo vingi vya anga ya juu ikiwa ni pamoja na vituo vya anga ya juu. Hali isiyo ya kawaida ya Ionospheric inaweza kuvuruga ishara, wanasayansi wanasema.
Rada sita zenye zimefungwa katika Mkoa wa Jilin, Mkoa wa Mongolia ya Ndani na Mkoa wa Xinjiang kaskazini mwa China.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma