

Lugha Nyingine
China yaitaka Marekani kuacha kuitumia Taiwan kama nyenzo ya kuidhibiti China
BEIJING - Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Wang Wenbin siku ya Jumanne kwenye mkutano na waandishi wa habari wakati akijibu swali kuhusu "pongezi" za Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken kwa kiongozi mpya wa eneo la Taiwan ameitaka Marekani kuheshimu kwa dhati ahadi zake za kutoitumia Taiwan kama nyenzo ya kuidhibiti China, na kuacha kupuuza kanuni ya kuwepo kwa China moja.
Msemaji huyo amesema kile ambacho Marekani imefanya kinakiuka sana kanuni ya kuwepo kwa China moja na taarifa tatu za pamoja za China na Marekani, na inakiuka dhamira yake ya kisiasa ya kudumisha tu uhusiano wa kitamaduni, kibiashara na mwingine usio rasmi na eneo la Taiwan. Hii inatoa ishara yoyote ya makosa kwa vikundi vya nguvu ya mafarakano ya kuifanya "Taiwan ijitenge". China inasikitishwa sana na kupinga, na imewasilisha malalamiko mazito kwa Marekani.
Kuna China moja tu duniani. Taiwan ni sehemu isiyoweza kutengwa ya nchi ya China. Suala la Taiwan ni kiini cha maslahi ya China na ni mstari mwekundu wa kwanza ambao haupaswi kuvukwa katika uhusiano wa China na Marekani, amesisitiza.
"China inapinga vikali mawasiliano ya kiserikali ya aina yoyote kati ya Taiwan na Marekani na inapinga Marekani kuingilia masuala ya Taiwan kwa namna yoyote au kwa kisingizio chochote," msemaji huyo amesema.
China inaitaka Marekani kurekebisha makosa yake mara moja, kufanyia kazi dhamira ya Rais Joe Biden ya kutounga mkono "Taiwan ijitenge," "China mbili" au "China moja, Taiwan moja" na kutotumia Taiwan kama nyenzo ya kuidhibiti China, kuacha kupotosha na kupuuza kanuni ya kuwepo kwa China moja, kuacha kutia moyo na kuunga mkono vikundi vya nguvu ya mafarakano ya kutaka "Taiwan ijitenge" kwa namna yoyote ile na kuacha kuvuruga amani na utulivu katika Mlango-Bahari wa Taiwan.
Kuifanya "Taiwan ijitenge" hakutapata njia popote na mtu yeyote anayetia moyo na kuunga mkono " Taiwan ijitenge" atashindwa. Hakuna uingiliaji wa nje unaoweza kurudisha nyuma mwelekeo wa Mungano wa China. Jaribio lolote la kupinga kanuni ya kuwepo kwa China moja na kuhatarisha mamlaka ya nchi na ukamilifu wa ardhi ya China litapata majibu makali ya kithabiti ya China, ameongeza.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma