

Lugha Nyingine
J.P. Morgan yaongeza makadirio ya ukuaji wa uchumi wa China Mwaka 2024 hadi asilimia 5.2
Picha hii iliyopigwa tarehe 4 Novemba 2023 ikionyesha mwonekano wa Mji wa Shanghai, Mashariki mwa China. (Xinhua/Wang Jianhua)
SHANGHAI - Zhu Haibin, mwanauchumi mkuu wa China katika Kampuni ya kimataifa ya mambo ya fedha na uchumi ya J.P. Morgan, amekadiria kuwa uchumi wa China utakua kwa asilimia 5.2 Mwaka 2024, kutoka asilimia 4.9.
Mwanauchumi huyo ametangaza makadirio yake hayo yaliyohuishwa kwenye Mkutano wa kilele wa Kimataifa wa J.P. Morgan China mjini Shanghai siku ya Jumatano.
Zhu amesema kuwa ukuaji wa uchumi wa China kwa asilimia 5.3 katika robo ya kwanza ya Mwaka 2024 nizaidi ya matarajio ya soko na kuashiria mwanzo mzuri wa mwaka.
Amebainisha kuwa mambo makuu matatu muhimu ya uchumi wa China katika robo ya kwanza ya mwaka ni thamani ya ongezeko la viwanda imeongezeka kuliko mwaka jana wakati kama huo, kiasi ambacho kinazidi ukuaji wa jumla wa uchumi wa nchi hiyo, pamoja na kuwa na bidhaa mbalimbali zinazouzwa maeneo mbalimbali nje ya nchi, na kuibuka kwa teknolojia mpya na viwanda vipya kama vichocheo vya ukuaji wa uchumi.
Zhu amesema anakadiria kiwango cha ubadilishaji wa renminbi, sarafu ya China, kubaki imara kwa kiasi kikubwa mwaka mzima. "Ingawa yuan ya China inakabiliwa na shinikizo la kushuka kwa thamani kwa muda mfupi dhidi ya dola ya Marekani, shinikizo la kushuka litapunguzwa kwani Benki Kuu ya Marekani huenda ikapunguza viwango vya riba katika nusu ya pili ya mwaka," amesema.
Mkutano wa Kilele wa Kimataifa wa J.P. Morgan China ni mojawapo ya mikusanyiko mikubwa na yenye ushawishi mkubwa zaidi ya kila mwaka ya viongozi wa biashara nchini China, inalenga kuunganisha jumuiya ya kimataifa ya uwekezaji na soko la China. Mwaka huu ni mwaka wa 20 mfululizo kufanyika kwa mkutano huo.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma