

Lugha Nyingine
Waziri wa Usalama wa Umma wa China akutana na waziri wa mambo ya ndani wa Burundi
Waziri wa Usalama wa Umma wa China, Wang Xiaohong akikutana na Martin Niteretse, waziri wa mambo ya ndani, maendeleo ya jamii na usalama wa umma wa Burundi, mjini Beijing, China, Mei 22, 2024. (Xinhua/Yue Yuewei)
BEIJING - Waziri wa Usalama wa Umma wa China, Wang Xiaohong amekutana na Martin Niteretse, waziri wa mambo ya ndani, maendeleo ya jamii na usalama wa umma wa Burundi siku ya Jumatano mjini Beijing, akisema kuwa China ingependa kufanya juhudi pamoja na Burundi katika kuimarisha urafiki na kuongeza hali ya kuaminiana kwa pande mbili, kuendeleza kwa kina ushirikiano wa kunufaishana wa kufuata hali halisi, na kuimarisha ushirikiano wa usalama chini ya mfumo wa ushirikiano wa Ukanda Mmoja, Njia Moja.
Amesema, nchi hizo mbili pia zinapaswa kukabiliana kwa pamoja na uhalifu wa kuvuka mipaka, kuongeza kwa pande zote usimamizi wa utekelezaji wa sheria na ushirikiano wa usalama, na kuweka mazingira salama na mazuri kwa maendeleo ya kiuchumi na kijamii ya nchi hizo mbili.
Niteretse amesema kuwa Burundi ingependa kuimarisha mabadilishano na mawasiliano na China na kuzidisha ushirikiano katika utekelezaji wa sheria na usalama.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma