Jeshi la Ukombozi wa Umma la China lafanya mazoezi ya pamoja ya kijeshi kuzunguka Kisiwa cha Taiwan

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Mei 23, 2024

NANJING - Kamandi ya Kivita ya Mashariki ya Jeshi la Ukombozi wa Umma la China (PLA) imefanya mazoezi ya pamoja ya kijeshi kuzunguka kisiwa cha Taiwan kuanzia saa 1:45 asubuhi ya leo Alhamisi ambapo mazoezi hayo yanafanyika katika Mlango Bahari wa Taiwan, kaskazini, kusini na mashariki mwa kisiwa cha Taiwan, pamoja na maeneo karibu na visiwa vya Kinmen, Matsu, Wuqiu, na Dongyin.

Li Xi, Msemaji wa kamandi hiyo, amesema vikosi vya kijeshi vikiwa pamoja na jeshi la nchi kavu, jeshi la majini, jeshi la angani na kikosi cha roketi cha kamandi hiyo vimepangwa kufanya mazoezi ya pamoja, yaliyopewa jina la Upanga wa Pamoja -2024A, kuanzia leo Alhamisi hadi Ijumaa.

Mazoezi hayo yanawekwa mkazo katika kufanya doria ya pamoja ya utayari wa kupambana angani na baharini, kunyakua kwa pamoja udhibiti kamili wa medani ya vita, na kufanya mashambulizi ya pamoja ya kulenga kwa usahihi maeneo lengwa muhimu, Li amesema, huku akiongeza kuwa mazoezi hayo yanahusisha doria ya meli na ndege zinazofunga maeneo karibu na kisiwa cha Taiwan na oparesheni fungamani ndani na nje ya mnyororo wa kisiwa hicho ili kujaribu uwezo wa pamoja wa vikosi vya kamandi hiyo wa kufanya mapambano.

Msemaji huyo amesema mazoezi hayo pia yanatumika kama adhabu kali kwa vitendo vya mafarakano vya kuifanya " Taiwan ijitenge" na kutoa onyo kali dhidi ya uingiliaji na uchochezi wa vikundi vya nje.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha