

Lugha Nyingine
Norway, Ireland na Hispania zatangaza kutambua rasmi nchi ya Palestina
Picha hii iliyopigwa kwenye skrini ya video iliyotolewa na Serikali ya Norway inamuonyesha Waziri Mkuu wa Norway Jonas Gahr Store akihudhuria mkutano na waandishi wa habari huko Oslo, mji mkuu wa Norway, Mei 22, 2024. (Serikali ya Norway/ Xinhua)
OSLO - Norway, Ireland na Hispania zimetangaza Jumatano kwamba zitaitambua rasmi Palestina kuwa nchi huru. Akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari huko Oslo, Waziri Mkuu wa Norway Jonas Gahr Store amesema Norway inaunga mkono kuipa Palestina hadhi ya nchi mwanachama kamili katika Umoja wa Mataifa (UN).
Norway inatambua rasmi Palestina kuwa nchi huru kuanzia tarehe 28 Mei. Hakutakuwa na amani katika Mashariki ya Kati bila suluhu ya nchi mbili. Na hatawezi kuwa na suluhu ya nchi mbili bila kuwepo nchi ya Palestina. Kwa maneno mengine, nchi ya Palestina ni sharti la kutimiza amani katika Mashariki ya Kati," Store amesema.
Amefafanua zaidi kwamba mipaka kati ya Palestina na Israel inapaswa kuwekewa juu ya mipaka iliyothibitishwa kabla ya Mwaka 1967, na Jerusalem ikiwa ni mji mkuu wa nchi zote mbili. Msimamo huu hautaathiri kufikia suluhu ya mwisho kwenye mipaka, ambayo inaweza kuhusisha kubadilisha ardhi.
Siku hiyo hiyo, Waziri Mkuu wa Ireland Simon Harris na Waziri Mkuu wa Hispania Pedro Sanchez walithibitisha kuwa nchi zao zitaungana na Norway katika kutambua Palestina.
"Leo Ireland, Norway na Hispania zinatangaza kwamba tunatambua nchi ya Palestina, kila mmoja wetu atachukua hatua zozote za kitaifa zinazohitajika kutekeleza uamuzi huo," Harris amesema huko Dublin, mji mkuu wa Ireland.
Ikulu ya Palestina siku hiyo ya Jumatano ilikaribisha kutambuliwa huko. Katika taarifa iliyochapishwa na shirika la habari la Palestina WAFA, uongozi wa Palestina umesema kwamba unathamini sana mchango wa Norway, Ireland na Hispania katika "kutoa haki ya watu wa Palestina ya kujiamuliwa juu ya ardhi yao na kuchukua hatua za kuunga mkono." utekelezaji wa suluhu ya nchi mbili."
Mtu akipita mbele ya bendera ya Palestina huko Oslo, mji mkuu wa Norway, Mei 22, 2024. (Picha na Chen Yaqin/Xinhua)
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa likifanya mkutano kuhusu hali ya Gaza kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York, Mei 20, 2024. (Manuel Elias/Picha ya Umoja wa Mataifa/ Xinhua)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma