Katibu Mkuu wa UN atoa wito wa mchango wa Afrika katika usanifu wa mfumo wa amani na usalama wa Dunia

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Mei 24, 2024

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, (UN) Antonio Guterres (Mbele) akiongea katika mkutano wa baraza la usalama kwenye makao makuu ya UN huko New York, Mei 23, 2024. (Manuel Elias/Picha ya UN / Xinhua)

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, (UN) Antonio Guterres (Mbele) akiongea katika mkutano wa baraza la usalama kwenye makao makuu ya UN huko New York, Mei 23, 2024. (Manuel Elias/Picha ya UN / Xinhua)

UMOJA WA MATAIFA - Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres siku ya Alhamisi wakati wa mjadala wa wazi wa Baraza la Usalama juu ya kuimarisha mchango wa Afrika katika kukabiliana na changamoto za usalama na maendeleo ya Dunia, amesema kuna haja ya kuuweka ushiriki na uongozi wa Afrika katika mfumo wa amani na usalama wa Dunia.

Baada ya Vita vya Pili vya Dunia, mifumo ya usimamizi wa Dunia, pamoja na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa. ilibuniwa na nchi zenye nguvu kubwa zaidi wakati huo, ambapo nchi nyingi za Afrika zilikuwa bado ziko katika harakati za kutupa minyororo ya ukoloni. Kuanzia wakati huo, mabadiliko yametokea katika Dunia, lakini vyombo vya Dunia havijabadilika, amesema.

"Leo, nchi za Afrika zinaendelea kukataliwa kiti kwenye meza ya mazungumzo, pamoja na baraza hili. Athari za muundo huu usio na usawa ni wazi kuziona," amesema.

Afrika inastahili sauti katika mfumo wa amani na usalama wa Dunia. Lakini kuimarisha sauti ya Afrika kunaweza kutokea tu ikiwa nchi za Afrika zinaweza kushiriki kwa usawa katika muundo wa usimamizi wa Dunia, amesema. "Hii lazima ijumuishe kurekebisha ukosefu wa uwakilishi wa kudumu wa Afrika katika Baraza la Usalama. Na lazima ijumuishe kufanya mageuzi ya mfumo wa mambo ya fedha wa Dunia, haswa kazi yake ya kushughulikia madeni, ili nchi za Afrika ziwe na uungaji mkono zinaouhitaji kupanda ngazi ya maendeleo."

Mkutano wa Kilele wa Siku za Baadaye wa mwezi Septemba itakuwa fursa ya kuhimiza masuala haya yote, amesema.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, (UN) Antonio Guterres (Katikatie) akiongea katika mkutano wa baraza la usalama kwenye makao makuu ya UN huko New York, Mei 23, 2024. (Manuel Elias/Picha ya UN / Xinhua)

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Renato Lu)

Picha