

Lugha Nyingine
Mjumbe maalum wa Rais wa China ahudhuria hafla ya kuapishwa kwa Rais wa Visiwa vya Comoro
MORONI - Kwa mwaliko wa Rais Azali Assoumani wa nchi ya Visiwa vya Comoro, Mjumbe Maalum wa Rais Xi Jinping wa China He Baoxiang amehudhuria hafla ya kuapishwa kwa Azali mjini Moroni siku ya Jumapili.
He, ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kitaifa ya Baraza la Mashauriano ya Kisiasa ya Umma ya China, alikutana na Azali huko Moroni, mji mkuu wa Visiwa vya Comoro siku ya Jumamosi.
Mjumbe huyo aliwasilisha salamu za pongezi na za kila kheri za Rais Xi kwa Rais Azali, akisema kuwa China inathamini sana maendeleo ya uhusiano kati yake na Visiwa vya Comoro.
Amesema China inapenda kushirikiana na Visiwa vya Comoro kutekeleza makubaliano muhimu yaliyofikiwa na wakuu wa nchi hizo mbili, kusaidiana kithabiti katika kulinda maslahi ya msingi, kuendeleza ushirikiano wa Ukanda Mmoja, Njia Moja, kuimarisha ushirikiano wenye matokeo halisi katika sekta mbalimbali ndani ya mifumo ya Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika na Baraza la Ushirikiano kati ya China na Nchi za Kiarabu, kwa lengo la kuinua urafiki wa jadi kati ya nchi hizo mbili kwenye ngazi mpya.
Kwa upande wake Rais Azali ametoa shukrani zake kwa Rais Xi kwa kutuma mjumbe maalum kuhudhuria hafla ya kuapishwa kwake na kumwomba He kuwasilisha heshima yake ya juu na salamu za dhati kwa Rais wa China.
Nchi ya Visiwa vya Comoro inathamini uungaji mkono mkubwa wa muda mrefu wa China kwa maendeleo ya taifa lake na kuenzi urafiki wa jadi kati ya nchi hizo mbili, Rais Azali amesema.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma