

Lugha Nyingine
Nyangumi aliyekwama pwani arudi baharini huko Hainan, China
Nyangumi kiongozi mwenye pezi fupi Haitang aliyekwama akihamishwa kwenye meli ya utafiti siku ya Jumamosi na kurudishwa baharini saa 12:15 asubuhi siku ya Juampili. (Picha na Wang Chenglong/Ilichapishwa na chinadaily.com.cn)
Baada ya kutunzwa kwa miezi sita, nyangumi kiongozi mwenye pezi fupi aitwaye Haitang alirudishwa baharini kwenye Mkoa wa Hainan, China siku ya Jumapili.
Haitang aligunduliwa kujeruhiwa na kukwama kwenye Ghuba ya Haitang mjini Sanya tarehe 3, Januari. Kutokana na utunzaji mzuri wa Kituo cha Hifadhi ya Wanyama cha Sanya Haichang, nyangumi huyu alirejea kwenye hali ya afya njema na kuwa tayari kurudi baharini.
Chini ya uangalifu wa madaktari na wataalamu, chakula cha nyangumi huyu kwa kila siku kiliongezeka kuwa na ngisi kilogramu 12 na samaki ya herring kilogramu 2. Urefu wake ulikua hadi mita 3.7 kutoka mita 3.6, na kifua chake kilipanua kutoka mita 1.9 hadi mita 2.
“Ngisi ni muhimu kwa nyangumi viongozi,” alisema Cao Zheng, kiongozi wa kituo hicho cha hifadhi. “Haitang amefanya mazoezi ya kutafuta samaki majini na anatakiwa kuzoea vizuri idadi kubwa ya ngisi karibu na Sanya.”
Kifaa maalumu kitafuatilia mwendo wa Haitang baada ya kurudi baharini. Timu husika imepanga vizuri mchakato wa kumrudisha, ukihusisha kupanga usafiri na kuchagua mahali panapofaa ambapo nyangumi waliwahi kutembea. Sehemu yake ya kurudi ipo zaidi ya kina cha mita 500 kutokea juu ya uso wa bahari, hali ambayo inakidhi mahitaji ya nyangumi huyu mwenye uzito wa kilogramu 500.
“Kwa kumrudisha Haitang kwenye makazi anayoyafahamu pamoja na nyangumi wengine, tunatakia atajiunga kwa mafanikio na jumuiya yake mpya,” alisema Cao.
“Haitang” akirudi nyumbani chini ya uangalifu wa droni, baada ya utunzaji wa binadamu wa siku 145. Ili kufuatilia na kuangalia hali yake, wanasayansi wameambatisha kifaa maalumu kwenye mgongo wake. (Picha na Wang Chenglong/Ilichapishwa na China Daily)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma