Waziri Mkuu wa China aitaka Japan kuendana na China katika mwelekeo mmoja

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Mei 27, 2024

Waziri Mkuu wa China Li Qiang akikutana na Waziri Mkuu wa Japan Fumio Kishida pembezoni mwa Mkutano wa tisa wa Kilele wa Pande Tatu kati ya China, Japan na Jamhuri ya Korea, mjini Seoul, Korea Kusini, Mei 26, 2024. (Xinhua/Liu Bin)

SEOUL - Waziri Mkuu wa China Li Qiang Jumapili kwenye mkutano wake na Waziri Mkuu wa Japan Fumio Kishida pembezoni mwa Mkutano wa tisa wa Kilele wa Pande Tatu kati ya China, Japan na Jamhuri ya Korea ametoa wito kwa Japan kufanya kazi na China katika mwelekeo mmoja na kutekeleza makubaliano muhimu yaliyofikiwa na viongozi wa nchi hizo mbili.

"Inatarajiwa kuwa nchi hizo mbili zitaendelea kuimarisha hali ya kuaminiana, kupanua ushirikiano, kudhibiti ipasavyo tofauti, na kujenga uhusiano wa kiujenzi na kithabiti kati ya China na Japan unaokidhi matakwa ya zama mpya," Li amesema.

Li amesema mwezi Novemba mwaka jana, Rais Xi Jinping wa China na Waziri Mkuu Kishida walikutana mjini San Francisco, na kufikia makubaliano muhimu, na kusisitiza msimamo wa kuendeleza kwa pande zote uhusiano wa kimkakati na wa kunufaishana kati ya China na Japan, na kutoa mwongozo muhimu wa kisiasa kwa maendeleo ya uhusiano wa pande mbili.

Suala la historia na suala la Taiwan ni masuala makuu kuhusu msingi wa kisiasa wa uhusiano wa China na Japan, vilevile ni masuala ya msingi ya imani na uadilifu, na suala la Taiwan ni msingi wa maslahi makuu na mstari mwekundu wa China, amesema.

Inatarajiwa kuwa Japan itaheshimu ahadi yake na kujenga mazingira mazuri kwa ajili ya maendeleo endelevu ya uhusiano kati ya pande mbili, amesema Li.

“China na Japan zinapaswa kusaidiana kufanikiwa, kudumisha kwa pamoja mnyororo wa viwanda na usambazaji ulio imara na usiozuiliwa, na kulinda mfumo wa biashara huria duniani,” amesema.

Kutolewa kwa maji chafu ya nyuklia ya Fukushima kunabeba wajibu juu ya afya ya binadamu, mazingira ya bahari ya kimataifa na maslahi ya kimataifa ya umma, Li amesema.

Huku akibainisha kuwa China ni mdau mkubwa, na serikali na watu wa China wana wasiwasi mkubwa juu ya suala hilo, Li amesema China inatumai Japan itaonyesha zaidi nia dhati na msimamo wa kiujenzi juu ya masuala mbalimbali kuhusu suala hilo.

Kwa upande wake, Kishida amesema kudumisha kasi nzuri ya maendeleo ya uhusiano kati ya Japan na China siyo tu kwamba kuna nufaisha nchi zote mbili, bali pia kunanufaisha dunia nzima.

Amesema Japan ingependa kushirikiana na China kutekeleza makubaliano muhimu yaliyofikiwa na viongozi wa nchi hizo mbili, kudumisha mawasiliano ya ngazi ya juu na kuimarisha ushirikiano katika sekta mbalimbali.

Waziri Mkuu wa China Li Qiang akikutana na Waziri Mkuu wa Japan Fumio Kishida pembezoni mwa Mkutano wa tisa wa Kilele wa Pande Tatu kati ya China, Japan na Jamhuri ya Korea, mjini Seoul, Korea Kusini, Mei 26, 2024. (Xinhua/Liu Bin)

Waziri Mkuu wa China Li Qiang akikutana na Waziri Mkuu wa Japan Fumio Kishida pembezoni mwa Mkutano wa tisa wa Kilele wa Pande Tatu kati ya China, Japan na Jamhuri ya Korea, mjini Seoul, Korea Kusini, Mei 26, 2024. (Xinhua/Liu Bin)

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha