Maadhimisho ya Siku ya Afrika yafanyika huku wito ukitolewa kutekelezwa kwa matarajio ya kuanzishwa kwa AU

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Mei 27, 2024

Picha hii iliyopigwa Februari 17, 2024 ikionyesha mandhari ya nje ya makao makuu ya Umoja wa Afrika (AU) mjini Addis Ababa, Ethiopia. (Xinhua/Li Yahui)

Picha hii iliyopigwa Februari 17, 2024 ikionyesha mandhari ya nje ya makao makuu ya Umoja wa Afrika (AU) mjini Addis Ababa, Ethiopia. (Xinhua/Li Yahui)

ADDIS ABABA - Bara la Afrika limeadhimisha Siku ya Afrika Jumamosi kwa wito wa kufikia matarajio ya kuanzishwa kwa Umoja wa Afrika (AU) ambapo Moussa Faki Mahamat, Mwenyekiti wa Kamisheni ya AU, katika ujumbe wake kwenye maadhimisho hayo ya mwaka huu, amesema tangu kuundwa kwa OAU, Bara la Afrika "limejikomboa kutoka kwa ukoloni na mfumo wa kutisha wa ubaguzi wa rangi. Rasilimali zake za kiakili, kisayansi na kitamaduni zimeendelezwa sana, kuwa za aina mbalimbali na zilizojaa utajiri."

Huku akibainisha kuwa uchumi wa bara hilo umekua kwa viwango vinavyoonewa wivu na sehemu nyingi za dunia, mkuu huyo amesema uhimilivu wa Afrika wakati wa janga la UVIKO-19 uliwaajabisha watu.

"Kuongezeka kwa kasi kwa idadi ya watu barani Afrika, vikwazo vyake vya kijamii ambavyo vinaenda kinyume na mahitaji ya Dunia Mpya, kuendelea kuwa mbaya kwa hali ya hewa, aina mbalimbali za uingiliaji wa nje katika masuala yetu ya ndani, upenyezaji wa baadhi ya watu kwa maneno ya kigeni; na mapungufu ya wazi katika masuala ya utawala havijasaidia kugeuza maendeleo mazuri yaliyotajwa hapo juu kuwa mambo ya haki ya kijamii, usawa na ustawi jumuishi,” amesema.

Faki amesema maadhimisho ya Siku ya Afrika ni "wakati mwafaka wa kutafakari ili kutathmini umbali ambao tumefikia na kutafakari juu ya njia mbele yetu."

"OAU iliyozaliwa kwenye mapambano yetu, sasa iko njia panda, lazima tujifanyie mageuzi kithabiti na kwa ujasiri ili tuwe vile waasisi wetu walivyotaka tuwe, ambayo ni kuwa chachu yenye nguvu ya umoja, ukombozi, ufungamanishaji na kutetea heshima ya Mwafrika kuhusiana na sisi wenyewe na wengine,” amesema.

Wizara ya Mambo ya Nje ya Ethiopia imesema shughuli hiyo inaadhimisha "urithi wetu, umoja na nguvu wa pamoja wa Waafrika."

"Ni wakati wa kutafakari uzoefu wetu wa pamoja na kuweka azma mpya kujenga Afrika yenye haki, ustawi na umoja," wizara hiyo imesema katika taarifa yake iliyotolewa Jumamosi.

Siku ya Afrika inaadhimishwa kila mwaka Mei 25 ili kuadhimisha mafanikio ya Umoja wa Nchi Huru za Afrika (OAU), ambayo ni mtangulizi wa AU, tangu kuundwa kwake Mei 25, 1963.

Siku hiyo inaadhimishwa ili kutambua mchango wa umoja huo wa bara katika vita dhidi ya ukoloni na maendeleo ambayo Afrika imepiga, huku ikitafakari changamoto za pamoja ambazo bara hilo linakabiliana nazo katika mazingira ya kimataifa, kwa mujibu wa AU.

Watu kutoka Rwanda wakicheza ngoma kwenye hafla ya kuadhimisha Siku ya Afrika mjini Kampala, Uganda, Mei 25, 2024. (Picha na Nicholas Kajoba/Xinhua)

Watu kutoka Rwanda wakicheza ngoma kwenye hafla ya kuadhimisha Siku ya Afrika mjini Kampala, Uganda, Mei 25, 2024. (Picha na Nicholas Kajoba/Xinhua)

Watu waliovalia mavazi ya Kiafrika wakicheza ngoma wakati wa shughuli ya mawasiliao ya utamaduni ya China na Zimbabwe huko Goromonzi, ambayo ni jamii ya kijijini iliyoko Jimbo la Mashonaland Mashariki, Zimbabwe, Mei 23, 2024. (Xinhua/Tafara Mugwa)

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha