Mashindano ya Daraja la Lugha ya Kichina yafanyika nchini Ghana ili kuchagua vijana hodari kuzungumza lugha hiyo

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Mei 27, 2024

Watu wakishiriki kwenye mtihani wa maandishi wa mashindano ya 17 ya "Daraja la Lugha ya Kichina", ambayo ni mashindano ya lugha ya Kichina kwa wanafunzi wa shule za sekondari za nchi za kigeni, mjini Accra, Ghana, Mei 24, 2024. (Picha na Seth/Xinhua)

ACCRA - Mashindano ya kuchagua nchini Ghana kwenye mashindano ya 17 ya "Daraja la Lugha ya Kichina", ambayo ni mashindano ya lugha ya Kichina kwa wanafunzi wa shule za sekondari za nchi za kigeni, yamefanyika kwa mafanikio siku ya Ijumaa.

Mashindano hayo yaliyoandaliwa na Taasisi za Confucius katika Chuo Kikuu cha Ghana, Chuo Kikuu cha Cape Coast (UCC), na Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia cha Kwame Nkrumah, yamewakutanisha pamoja wahitimu wanane kutoka kote nchini humo.

Akihutubia kwenye hafla hiyo, Clement Appah, mkurugenzi wa Ghana wa Taasisi ya Confucius katika Chuo Kikuu cha Ghana, amesema shindano hilo ni daraja la utamaduni na lugha kati ya China na nchi nyingine. "Mashindano yanaashiria uhusiano na mawasiliano ya maarifa, utamaduni na urafiki."

"Kujifunza lugha ya Kichina na kujifunza utamaduni wake kutakutayarisha kwa mustakabali wa siku za baadaye ambao lugha ya Kichina inachukua nafasi kubwa na siku za baadaye ambazo utakuwa tayari kutumia fursa zote zinazotokana na kujua Lugha ya Kichina," mkurugenzi huyo wa Ghana ameongeza.

Margaret Amoabeng, mwanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Juu ya Maandalizi ya Chuo Kikuu ya UCC, amekuwa mshindi wa mashindano hayo, ambayo imemwezesha kushiriki katika mashindano ya kimataifa nchini China.

"Nimefurahi sana, na hata sijui jinsi ya kuelezea namna nilivyo na furaha. Kusema kweli, maandalizi yalikuwa magumu sana," amesema huku akiongeza kuwa atajiandaa kwa bidii zaidi kwa mashindano ya kimataifa nchini China ili kushinda tuzo kwa Ghana.

Mtu akitoa hotuba kwenye mtihani kwenye mashindano ya 17 ya "Daraja la Lugha ya Kichina", ambayo ni mashindano ya lugha ya Kichina kwa wanafunzi wa shule za sekondari za nchi za kigeni, mjini Accra, Ghana, Mei 24, 2024. (Picha na Seth/Xinhua)

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha